Raisi Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuongoza zoezi la kuzamisha baharini meli iliyotiwa mbaroni ikiwa imebeba dawa za kulevya mwezi uliopita.

uhuru at seaMaafisa wakuu wa usalama hapa Mombasa wataandamana na Uhuru kutekeleza zoezi hilo.

Akifungua rasmi maonyesho ya kimataifa ya kilimo hapa Mombasa hapo jana, Rais Kenyatta alisema meli hiyo itazamishwa baharini huku akiongoza kwamba bandari ya Mombasa kamwe haitotumika tena kupitisha dawa za kulevya

Alisisitiza kwamba serikali itakabiliana vilivyo na wanaoendesha biashara hiyo.

Kauli ya Raisi ilikuja saa chache tu baada ya jaji wa mahakama ya Mombasa MaxwellGicheru kuamuru kuharibiwa kwa dawa za kulevya aina ya Heroin zenye thamani ya shilingi bilioni moja zilizonaswa bandari mombasa mwezi jana.

 

Add a comment (0)

Michezo

Michuano ya ngano ni taifa super cup inaendelea leo baada ya pumziko la hapo jana hii leo jumapili Green Eagles watamenyana na Shell Beach katika uga wa MSC.

 

 

Ronaldo alituzwa tuzo la mchezaji bora ulaya hivi majuzi alifanya mzaha alipodai iwapo angetoa kauli yake awali angepelekwa jela.

HASIMU

Kauli ya Ronaldo inajiri miezi michache baada ya aliyekua sogora wa Argentina Diego Maradona kudai kwamba FiFa ilidanganya kumpa Messi tuzo hilo akisema messi hakustahiki.

Messi aliiongoza Argentina hadi fainali na kushindwa na Ujerumani goli 1 kwa nunge.

Haya yanajiri baada ya Falcao kuachwa nje ya kikosi cha Monaco kilichotoka sare ya goli 1 kwa 1 na lille hapo jana jumamosi licha ya kujumlishwa katika kikosi hicho awali.

Vilabu vinavyomngangania ni pamoja na Manchester City,Juventus,Arsenal na Real Madrid.

Falcao

 

New Castle wakatoshana nguvu na Crystall palace magoli 3 kwa 3 ,

Swansea iliendelea vyema ikipata ushindi wake wa 3 kwa kuilza Westbromwich Albion magoli 3 bila jibu,

Qpr ikailaza Sunderland goli 1 bila jibu, Southampton ikailaza Westham magoli 3 kwa 1.

MECHI ZA LEO JUMAPILI:

ASTON VILLA NA HULL

TOTTENHAM NA LIVERPOOL

LEICESTER CITY NA ARSENAL

 

Goli hilo la kipekee lilitiwa kimiani na mchezaji Mame Biram Diouf kunako dakika ya 58.

Stoke walikua hawajapata ushindi katika mechi zao 12 jijini Mancheste yaani si Old Trafford wala Etihaad lakini jana wakajinafas.

Dioff

(GOLI LAKE NA LA KIPEKEE DIOUF)

International News

Ofisi  ya katibu  mkuu   wa  Umoja  wa  Mataifa  Ban Ki-moon  katika taarifa  imesema  walinzi  hao  wa  amani , kutoka  taifa  la Fiji  katika  bahari  ya  Pacific , walikamatwa  mapema  jana katika  upande  wa  Syria  wa  milima  ya  Golan katika  mapigano  kati  ya  watu  wenye  silaha  na  majeshi ya  serikali  ya  Syria.

Taarifa  hiyo  haikufafanua  kundi gani  lenye  silaha  linawashikilia  walinzi  hao  wa  amani.

Makundi  kadhaa  ya  waasi  nchini  Syria , ikiwa  ni  pamoja na  kundi  lenye  mafungamano  na  al-Qaeda   la  Nusra Front , yamekuwa  yakipigana  na  jeshi  la  Syria  karibu na  milima  ya  Golan.

Siku  ya  Jumatano , wapiganaji  wa upinzani  walikamata  kivuko  katika milima  ya  Golan katika  mpaka  unaogombani  kati  ya  Israel  na  Syria.

 

Marekani na Umoja wa Mataifa pia zimeyakaribisha makubaliano hayo ya kusitisha mapigano yaliyosubiriwa kwa muda mrefu ambayo yalifikiwa na Waisrael na Wapalestina.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema anataraji kuwa mpango huo utaruhusu mchakato wa kisiasa wa kupatikana amani ya kudumu katika eneo hilo.

Misri ambayo iliongoza juhudi hizo za mapatano, imesema mazungumzo yayiso ya moja kwa moja baina ya Israel na wanamgambo yapaswa kuendelea katika kipindi cha mwezi mmoja.

Imesema vivuko vyote baina ya Gaza na Israel vitafunguliwa ili kurahisisha shughuli za kiutu na msaada wa dharura pamoja na ujenzi.

 

 

 

Kundi la Hamas limethibitisha kurefushwa kwa muda huo lakini limeilaumu Israel kwa ukaidi katika mazungumzo hayo magumu.

Muda wa siku tano za usitishwaji mapigano uliowekwa hapo kabla ulitarajiwa kumalizika saa sita usiku wa kuamkia leo saa za Gaza.

Umoja wa Mataifa umejitolea kuzikagua bidhaa za ujenzi zinazopelekwa Gaza ili kupunguza wasiwasi wa Israel kwamba bidhaa hizo huenda zikatumiwa kujengea tena mahandaki.

Hatua hiyo imefikiwa muda mchache kabla ya kumalizika kwa muda wa kusitisha mapigano kwa mara ya pili na baada ya Israel kuripoti roketi moja limerushwa kutoka Gaza, nayo kujibu kwa kushambulia maeneo kadhaa kwenye Ukanda wa Gaza.

Hamas imekanusha kurusha roketi lolote kuelekea Israel, na imeilaumu Israel kwa kuvunja makubaliano ya kusitisha mapigano.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema mpango huo wa kusitisha mashambulizi unaanza kutekelezwa leo asubuhi, na kudumu kwa kipindi cha saa 72, au urefushwe zaidi.

Wakati wa kipindi hicho, majeshi ya Israel yatasalia tu katika maeneo yaliko.

Amesema wajumbe wa Israel na Palestina wataelekea mara moja mjini Cairo kufanya mazungumzo na serikali ya Misri, chini ya mwaliko wa nchi hiyo, yanayolenga kufikia makubaliano ya kusitishwa kabisa mashambulizi.

Wakati wa mazungumzo hayo, pande zote mbili zitaweza kuyaangazia waziwazi masuala muhimu yanayozihusu.

Mkuu  wa  idara  ya misaada  ya  dharura  ya  Umoja  wa  mataifa  Valerie Amos  amesema  kuwa pande  zote  mbili  Israel  na  Hamas  zinapaswa  kuangalia  sheria  na kanuni  za  mapigano.

Zaidi ya wapalestina 1,400 wameuawa katika Ukanda wa Gaza tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi Julai 8.

Wanajeshi wa Israel wasiopungua 60 pamoja na raia watatu pia waliuawa.

Radio Rahma Twitter Feed

Like us in Facebook