Mchezaji kinda wa Kenya anayesakata soka ya kulipwa nchini Qatar Mohamed Katana almaarufu Messi amejiunga rasmi na klabu ya Sporting Lisbon ya nchini Ureno kwa mkataba wa miaka mitatu.

Shirika moja lisilo la kiserikali kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Kilifi limezindua mpango wa miaka mitano ambao unanuia kuimarisha afya ya uzazi katika kaunti hiyo.

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Lamu Shakila Abdalla amekashifu hatua ya serikali kuiwekea kaunti ya Lamu sheria ya kutotoka nje nyakati za usiku akisema kuwa sio suluhisho la usalama nchini.

Mahakama kuu jijini Nairobi imeagiza tume ya uchaguzi na mipaka kuanza upya harakati za utoaji upya wa zabuni kwa kampuni za kuchapisha karatasi za kura.

Idara ya watoto kaunti ndogo ya Ganze imesema kuwa visa vingi vya dhuluma dhidi ya wasichana wadogo vinaendelea kushuhudiwa kila mara eneo hilo.

Mtu mmoja amepoteza mkono wake na mwengine kupata majeraha mabaya ya kichwa baada ya Lori lililokuwa limebeba makasha kutoka bandari ya Mombasa kuelekea  taifa Jirani la Tanzania kupata ajali katika eneo la kitaruni huko Msambweni Kaunti ya kwale asubuhi ya leo.

Wauguzi katika kaunti ya Lamu wamefanya maandamano mjini Mpeketoni ili kushinikiza baraza la magavana na wizara afya kutia sahihi mkataba ya maelewano wa mwaka jana CBA.

Mwaniaji kiti cha ugavana kaunti ya Kilifi kupitia chama cha Kadu Asili Kazungu Kambi ameshtumu uongozi wa gavana wa sasa wa kaunti hiyo Amason Kingi akidai kuwa amekosa kutekeleza ahadi alizotoa katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2013.

Wagonjwa 25 waliokuwa wamelazwa katika hospitali kuu ya Nakuru wametoroka alasiri ya leo wakilalama kutotibiwa tangu jumatatu wakati  mgomo wa wauguzi ulipoanza leo ukiingia siku yake ya nne.

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Lamu Shakila Abdalla amekashifu kitendo cha maafisa wa polisi kuwapiga risasi vijana wawili nje ya mahakama ya Lamu na kutaka maafisa hao kutiwa mbaroni na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Daraja la Mbogolo kwenye barabara kuu ya Mombasa Malindi linakumbwa na tisho la kuvunjwa na maji baada ya mto Mbogolo kufurika maji kutokana na mvua kubwa ambayo inaendelea kunyesha katika kaunti ya Kilifi.

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir amezindua rasmi maktaba sita za kijamii za kisasa zilizojengwa na afisi ya hazina ya ustawishaji wa eneo bunge la Mvita, ili kuboresha viwango vya elimu katika eneo bunge hilo.

Kutokana na historia ya Lamu ya kutoweza kuwachagua viongozi wa kisasa wa jinsia ya kike, hali hii imetakwa kuwa moja wapo ya sababu ya Lamu kukosa maendeleo.

Kwa muda wakaazi wa Lamu wanalalama kwamba viongozi wao ambao ni waume tangu kupata Uhuru wa taifa, hawajawakilisha vizuri kupitia hazina mbali mbali za serikali.

Akiungumzia swala la uongozi wa wanawake, mwenyekiti wa Maendeleo ya wanawake kaunti ya Lamu Fatma Salim amesema taasubi ya kiume ndio imesababisha mwanamke wa Lamu kutoweza kuchaguliwa.

Fatma ameeleza kwamba viongozi wa jinsia ya kiume wamekuwa wakiingia uongozini na kusahau kutimiza ahadi zao hivyo basi kuitaka jamii ya Lamu kumpigia kura mwanamke katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa sababu wanawake wanatimiza ahadi.

Katika historia ya Lamu kiongozi wa kisiasa wa jinsia ya kike ni Shakila Abdallah ambaye kwa mara ya kwanza ameteuliwa kupitia kura katika mwaka wa 2013 kutokana na katiba ambayo iliweka kiti kimoja kuweza kupiganiwa na wanawake pekee.

Katika serikali zilizopita Shakila amekuwa akiteuliwa kama mjumbe maalum baaada ya kuangushwa katika kura.

Pia katika bunge la serikali ya kaunti viongozi wa jinsia ya kike ni kutokana na kupewa viti maalum na vyama vyao vya kisiasa.

Ili kupata mabadiliko kwa kutekelezewa ahadi zao wakaazi wa Lamu wamehimizwa zaidi kumteua kiongozi wa kike katika nyadhifa mbali mbali. 

 

Shughuli za usafiri zimetatizika katika kijiji cha Jimba eneo bunge la Rabai Kaunti ya Kilifi mapema leo baada ya Mito kadhaa kufurika kutokana na mvua inayoendelea kunyesha katika sehemu mbalimbali humu nchini.

Wakaazi mjini Malindi wameamkia tukio la kutamausha baada ya kupata mwili wa mwanamume wa makamo amejitia kitanzi ndani ya kibanda cha chakula.

Mtu mmoja ameaga dunia alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Msambweni baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Darling huko Diani kaunti ya Kwale usiku wa kuamkia Leo.

Wawakilishi wa ukanda wa Pwani kwenye michezo ya shule za upili muhula wa kwanza kwenye mpira wa vikapu upande wa kina dada Kaya Tiwi wameeza kuhifadhi taji lake baada ya kuwalaza St. Brigid’s kwa alama 48 kwa 35.

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Kilifi ambaye pia anawania kiti cha ubunge wa Malindi kwa tiketi ya chama cha ODM Aisha Jumwa ametishia kukihama chama hicho endapo uchaguzi wa mchujo hautakuwa huru na wazi.

Serikali ya kaunti ya Kilifi imesema kuwa milioni kumi na sita kati ya milioni hamsini na moja zilizoibwa kwa njia ya mtandao katika kaunti ya Kilifi zitarudishwa kwa serikali hiyo.

Mkufunzi wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesisitiza kuwa atatangaza karibuni iwapo atasalia na klabu hiyo au ataiaga baada ya kuiongoza kwa miongo miwili.

Vijana wa Changamwe United ambao walipanda kwenye ligi ya daraja la kwanza humu nchini walijizoleya alama tatu za bure baada ya wapinzani wao kushindwa kufika ugenini.

Mahakama ya Mombasa imekubali ombi la Gavana wa Mombasa Hassan Ali Joho  la kutaka asitiwe mbaroni hadi pale uchunguzi wa  kesi  inayomkabili utakapokamilika.

Waumini wa  kiislam wamefanya maombi maalum katika uwanja wa Caltex huko Likoni ili kuiombea kaunti ya Mombasa na nchi kwa jumla kuwa na amani na usalama na kuondokewa na matatizo mbali mbali.

Maafisa wa polisi kutoka vitengo mbali mbali  wamefanikiwa kuwatia mbaroni  washukiwa 12 wa ulanguzi wa dawa za kulevya hapa Pwani.

Vijana wa kiislamu walionaswa na maafisa wa polisi walipokuwa wakiendeleza masomo ya dini ya kiislamu wameachiliwa huru.

Maafisa wa polisi mjini Kilifi wanawazuilia vijana ishirini na mmoja wanafunzi wa madrasa ambao walikuwa wakiendeleza mafunzo ya dini katika eneo la Chumani.

Idara ya usalama eneo la Diani imeanzisha uchunguzi kufuatia tukio la uvamizi wa kituo cha kukabiliana na mihadarati cha Teens Watch huko Diani kaunti ya Kwale.

Kesi ya matamshi ya chuki na uchochezi iliyokuwa inamkabili mwakilishi wa wanawake kaunti ya Mombasa Mishi Mboko imetupiliwa mbali baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.

Gavana wa Mombasa Hassan Joho amemkashifu raisi Kenyatta kwa kuzindua feri ya zamani katika kivuko cha Mtongwe badala ya kununua feri mpya.

Hali ya huzuni imetanda katika kijiji cha Mitangani kaunti ndogo ya Ganze baada ya  mzee mwenye umri wa miaka sitini na mitano kuuawa kwa kukatwa shingo nyumbani mwake.

Gavana wa kaunti ya Tana River Hussein Dado amefichua sababu za kumfanya kuhamia chama cha Jubilee kutoka kile cha Wiper.

Gavana wa Tana River Hussein Dado amekashifu vikali hatua ya gavana wa Mombasa Hassan Joho ya kutaka kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa huduma katika kivuko cha Mtongwe iliyokuwa inaongozwa na rais Uhuru Kenyatta mapema leo.

Gavana wa Tana River Hussein Dado pamoja na mwakilishi wanawake Halima Ware wamejiunga na chama cha Jubilee baada ya kuahasi chama cha Wiper.

Serikali imewasuta viongozi wa upinzani wanaodai kuwa serikali inajipigia debe kutumia miradi iliyotekelezwa kupitia misaada au mikopo kutoka kwa mashirika ya kimataifa.

Mbunge wa Mvita AbdulSwamad Sharif Nassir amekashifu kitendo cha mkuu wa polisi wa kituo cha Makupa kuwanyima kibali cha kufanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Mvita.

Mamia ya vijana waliojiunga na kundi la wanamgambo la Al-Shabaab wamejiondoa kwenye kundi hilo na kurejea  kisiri katika kaunti ya  Lamu.

Huku serikali kuu na baraza la magavana wakitoa vitisho vya kuwafuta kazi madaktari wanaoshiriki mgomo, madaktari wamedinda kurudi  kazini.

Shirikisho la kandanda nchini FKF tawi dogo la Mombasa linatarajiwa kuandaa hafla ya kuzituza timu zilizoshiriki michuano ya Super 8 Mombasa Premier League msimu wa mwaka 2016.

Mahakama ya shanzu imetishia kumuondolea mashtaka ya ugaidi mke wa marehemu Rogo na wasichana wengine watatu baada ya mashahidi kukosa kufika mahakamani.

Timu ya taifa ya raga kwa wachezaji saba kila upande almaaruu Shujaaz wameibuka mabingwa wa mkondo wa Vegas7s kwenye msururu wa ligi ya raga duniani.

Naibu kinara wa chama cha ODM ambaye pia ni gavana wa Mombasa Hassan Ali Joho amedai kuwa viongozi wanaokihama chama hicho ni wale waliopoteza umaarufu wa kisiasa kutoka kwa wananchi.

Jumla ya visa vitatu  vya wanafunzi kupigwa na kujeruhiwa  vibaya  na walimu katika shule za msingi huko Diani kaunti ya  Kwale vimetajwa kuripotiwa kila wiki katika idara ya watoto  licha ya serikali kupiga marufuku adhabu ya kiboko shuleni mwaka 2011.

Baada ya kulazwa kwa mabao matatu kwa moja kwenye mechi iliyopita vijana wa Jurgen Kloop Liverpool wamelipiza kisasi hicho kwa Arsenal.

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir ametangaza rasmi azma yake ya kuwania kiti cha ugavana ifikapo mwaka 2022. 

Watu wanaoishi na virusi vya ukimwi katika eneo la Mswambweni kaunti ya Kwale wanalalamikia uhaba wa dawa za kupunguza makali ya maradhi hayo ARVs  katika hospitali ya rufaa ya Msambweni kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa. 

Mkutano wa kisiasa wa Jubilee uliotarajiwa kuandaliwa katika uwanja wa Kongowea wa Aljebra umetibuliwa baada ya vijana kudai ni ngome ya NASA.

Mazungumzo yanaendelea kuona kwamba visima vya zamani vimefunguliwa tena kama njia moja ya kukabiliana na hali ya kiangazi katika mbuga ya wanyama pori ya Sarova Taita Hills eneo la Tsavo.

Mashetani wekundu wa Manchester United wameratibiwa kupepetana dhidi ya FC Rostov ya Urusi kwenye awamu ya 16 bora ya michuano ya Europa.

Kiungo wa kati wa Arsenal Santi Cazorla atakaa nje ya uwanja kwa kipindi chote kilichosalia cha msimu huu kutokana na jeraha la kifungo cha mguu. 

Miili ya wanafunzi wawili waliofariki maji siku ya jumatatu imepatikana huko Kitere kaunti ya Tana River.

Shughuli za kawaida zimekwama katika kaunti ya Kilifi baada ya vibarua na wauguzi wa serikali hiyo kugoma kwa kile walichodai kuwa ni kudhulumiwa na serikali hiyo.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe leo ametimiza miaka 93 tangu kuzaliwa akiapa kusalia madarakani licha ya umri mkubwa na kuwa na matatizo ya afya.

Baadhi ya viongozi wa chama cha ODM kaunti ya Kwale wamemteua Issa Boi Juma kakake mdogo marehemu seneta Boi Juma ili aweze kumrithi na kukisimamia kiti cha useneta cha Kwale katika uchaguzi mkuu mwezi Agosti mwaka huu.

Watu watatu wameuwawa kwa kukatwa mapanga katika visa tofauti katika wadi ya Mwereni huko Lungalunga kaunti ya Kwale.

Washukiwa watatu kati ya saba wa ugaidi waliokamatwa jana wameachiliwa huru baada ya uchunguzi kuonyesha hawahusiki na ugaidi.

Polisi mjini Mombasa wamenasa magunia matano ya Bangi katika mtaa wa Tudor inayogharimu takriban shilling milioni mbili.

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir amewataka wafungwa walioko katika jela baridi kujisajili kwa wingi kama wapiga kura ifikapo siku ya Jumatatu juma lijalo wakati maafisa wa IEBC watakapo zuru jela hiyo ili kutekeleza shughuli hiyo ya usajili.

Muungano wa vyuo vikuu UASU,umetangaza kuanza maandamano nchi nzima siku ya Jumatatu baada ya  mazungumzo kushindikana juu ya mkataba wa mwaka 2013-2017.

Vijana walikuwa wamejihami wametatiza  kongamano la kinara wa cord Raila Odinga eneo la Turkana Mashariki, hali iliyomfanya Raila kutoroka bila kuhutubia umma.


Wanyama pori wanaendelea kuwahangaisha wakaazi wa kijiji cha Mkunumbi kilichoko katika mji wa Mpeketoni kaunti ndogo ya Lamu Magharibi.

Kadhi mkuu humu nchini Sheikh Ahmed Sharif Muhdhar amepongeza juhudi ya serikali ya kukabiliana na ulanguzi wa mihadarati.

Vijana wa Arsene Wenger Arsenal wameanza vibaya mkondo wa kwanza wa michuano ya klabu bingwa barani ulaya baada ya kulazwa kwa mabao matano kwa moja mikononi mwa Bayern Munich.

Viongozi  7 wa madaktari waliofungwa kutumikia kifungo cha mwezi mmoja gerezani wataachiliwa huru mara moja ili kuendelea na mazungumzo.

Kamishna  wa  kaunti ya Kwale Kutswa Olaka amewahahakikishia zaidi ya waathiriwa 4,000 wa dawa za kulevya kuwa hawatahaingaishwa wala kukamatwa na serikali badala yake serikali itawakamata madalali pamoja na walanguzi wa dawa za kulevya nchini.

Serikali imetangaza hali ya ukame ambayo kwa sasa inaathiri kaunti 23 kame na baadhi ya maeneo mengine hapa nchini kuwa janga la kitaifa.

Raia takribani 90 wa Somalia na wawili wa Kenya wametimuliwa kutoka Marekani saa chache baada ya taarifa kuibuka kwamba Rais Donald Trump atakabiliana na watu wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.

Mwakilishi wa wadi mteule kutoka kaunti ya Mombasa Sarah Nyamvula ameaga dunia leo katika hospitali moja nchini India alikokuwa anapokea matibabu baada ya kuugua ugonjwa wa saratani.

Viongozi wa baraza la maimamu na wahubiri nchini CIPK wamekutana na kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Aden Duale na kujadiliana kuhusu mtaala wa wakiislamu pamoja na maendeleo yaliyopigwa na serikali ya Jubilee miongoni mwa masuala mengine.

Wananchi wametakiwa kutogusa au kula ndege pori au wanyama waliofariki kufuatia mkurupuko wa homa ya ndege katika nchi jirani ya Uganda.

Seneta wa Mombasa Hassan Sarai na mwenzake wa Makueni Mutula Kilonzo Jnr wamemlaumu raisi Kenyatta na magavana wote kwa kushindwa kumaliza mgomo wa madaktari kwa haraka.

Mratibu mkuu wa serikali ukanda wa pwani Nelson Marwa amejitokeza kukanusha madai ya Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho kuwa alikamtwa na polisi hapo jana na badala yake kusema kuwa gavana huyo alijipeleka mwenyewe katika kituo cha polisi cha Urban na kujizuia katika kituo hicho.

Wanachama wa Muungano wa wahadhiri wa vyuo vikuu UASU na ule wa wafanyikazi wa vyuo vikuu nchini  KUSU wametoa makataa ya siku saba kwa serikali kutekeleza mkataba wa maelewano waliotia sahihi mwaka 2013 la sivyo kushiriki mgomo.

Serikali kupitia halmashauri ya bandari ya Mombasa imepokea rasmi magari ya moshi 6 kutoka serikali ya china ikiwa ni katika harakati ya kuanzishwa kwa usafiri kutumia reli ya kisasa SGR inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi Juni mwaka huu.

Polisi wameanza msako wa kuwatafuta wakuu wa muungano wa madaktari KMPDU, baada ya agizo la kukamatwa kwao kutolewa jana.

Siku chache baada ya gavana wa Mombasa Hassan Joho na mwenzake wa Kilifi Amason Kingi kupokonywa walinzi wao na serikali,sasa hatua sawia na hiyo imechukuliwa dhidi ya spika wa bunge la Kilifi Jimmy Kahindi.

Wanasiasa wa mrengo wa Jubilee  kaunti ya Mombasa, wanazidi kumkashifu gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho, kuhusiana na kauli yake ya kumsuta hadharani raisi Kenyatta.

Wanafunzi wawili bora kutoka  kila shule iliyoko  eneo bunge la Mvita waliofanya vyema katika mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE  mwaka jana watafaidika na ufadhili wa masomo ya sekondari baada ya mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharrif Nassir kuahidi kuwalipia karo.

Madakatari wamepinga nyongeza ya mshahara waliongozwa na serikali na  badala yake kusisitiza kuendelea na mgomo wao.

Waziri wa elimu dkt Fred Matiang’i ametangaza rasmi matokeo ya mtihani wa kitaifa wakidato cha nne  KSCE ambapo ni watahiniwa 141 waliopata alama ya ‘A’ ikilinganishwa na watahiniwa 2,636 waliopata alama hiyo katika mtihani huo mwaka jana.

Licha ya gavana wa Kwale Salim Mvurya kutengwa na baadhi ya magavana wenzake baada ya kuhasi mrengo wa CORD, sasa Mvurya amesema kuwa Jumuiya ya Pwani bado ipo licha ya tofauti zao za kisiasa.

Aliyekuwa meya wa zamani jijini Mombasa Taib Ali Taib atakuwa wakwanza kufika mbele ya jopo linamsaka mwenyekiti mpya wa tume ya uchaguzi na mipaka –IEBC.

Tarehe 10 Disemba imeainishwa kuwa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu- Kuainishwa kwa siku hii kunakumbusha juhudi kubwa zilizofanywa kwa lengo la kuwafanya watu waheshimu haki za binadamu kote duniani, azimio kubwa likiwa kupambana na dhulma,kuondoa ubaguzi na kueneza uhuru.

Maswala ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2017 yametawala kwenye hafla ya kuadhimisha sikukuu ya 53 ya Jamhuri humu nchini iliyoongozwa na Raisi Uhuru Kenyatta katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Maelfu ya wagonjwa katika hospitali za umma humu nchini  wanahangaika bila matibabu kufuatia mgomo wa kitaifa wa madaktari na wahudumu wengine wa afya. 

Imebainika kwamba utendakazi wa aliyekuwa afisa mkuu wa wizara ya elimu, vijana na michezo kaunti ya Kilifi Adan Mohammed uliingiliwa pakubwa na katibu wa serikali ya kaunti hiyo daktari Owen Baya.

Imekuwa vifijo na nderemo katika shule ya msingi ya Aga khan Mombasa baada ya mwanafunzi wao Mohammed Hassan Ramadhan kuwa wakwanza kwa kupata alama ya 422 huku mwanafunzi wa pili akipata alama ya 415.

Polisi wamelazimika kufyatua risasi hewani kuwatawanya wananchi waliojawa na ghadhabu katika eneo la Mazeras kaunti ya Kilifi baada ya mwanamume mmoja kuaga dunia baada ya kugongwa na gari katika eneo hilo mapema leo.

Kiongozi wa chama cha Narc Kenya Martha Karua amekuwa mwenyeji wa rais Uhuru Kenyatta katika kaunti ya Kirinyaga wakati rais Uhuru alizuru eneo hilo kuanzisha miradi mbali mbali.

Wabunge katika muungano wa CORD watawasilisha mswada bungeni ambapo iwapo utapita basi utailazimisha serikali kuwalipa wafanyabiashara wake pesa zote kwa muda wa siku thelathini.

Huku serikali ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu mwakani, idara ya polisi imetaja maafisa wapya wa upelelezi pamoja na wakuu wa polisi wa utawala katika kaunti mbali mbali nchini.

Afisa mtendaji wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Ezra Chiloba amewataka wakenya wanaoishi nje ya nchi kuisaidia tume hiyo kwa kujiandikisha kwa wingi kama wapigaji kura.

Mahakama ya Mombasa imetishia kumchukulia hatua seneta wa Nairobi Mike Sonko iwapo atashindwa kumleta kotini kiongozi wa vuguvugu la MRC, Omar Mwamnwadzi.

Mali ya thamani isiyojulikana imeteketea baada ya moto mkubwa kuzuka kwenye kampuni moja ya gesi katika kijiji cha Kwamagongo huko Kasemeni kinango katika kaunti ya Kwale usiku wa kuamkia leo.

Kinara wa muungano wa CORD Raila Odinga amewataka magavana wengine nchini pamoja na Rais Uhuru Kenyatta kuiga mfano wa gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi kwenye vita dhidi ya ufisadi.

Naibu rais William Ruto ameusuta mrengo wa upinzani CORD akiwataka kupanga manifesto ya muungano huo na kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa wapiga kura badala ya kutumia tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kama kizingiti.

Kesi iliyowasilishwa na aliyekuwa kadhi mkuu nchini Sheikh Hammad Kassim kupinga makamishena wa wakfu wa kiislamu sasa imetupiliwa mbali na mahakama ya Mombasa.

Takwimu zilizopo zinaonesha kuwa uwanja wa siasa humu nchini na hata katika nchi nyingi za Kiafrika umetawaliwa na idadi kubwa ya wanaume ukilinganisha na wanawake.

Kutokana na huduma duni za kiafya katika hospitali za umma humu nchini, imekuwa nadra sana kwa viongozi wa kuu serikalini kutibiwa katika hospitali hizi.

Jumla ya wanajeshi 2,000 kutoka mataifa ya Uganda, Tanzania, Burundi, Rwanda na Jeshi la humu nchini KDF wamekusanyika katika eneo la Matuga kaunti ya Kwale kwa zoezi la kuiga oparesheni ya shambulizi la kigaidi (Drill) lililozinduliwa ramsi hii leo na waziri wa ulinzi Rachael Omamo huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni ushirikiano imara katika Afrika Mashirika.

Zaidi ya familia 300 zilizoathirika na baa la njaa na zinazoishi na virusi vya Ukimwi katika maeneo ya Kikoneni, Vitsangalaweni na Godo kaunti ndogo ya LungaLunga zimefaidika na chakula cha msaada kutoka kwa wahisani mbalimbali likiwemo shirika la kijamii la Fanikisha. 

Kiongozi wa chama cha NARC Kenya Martha Karua ameshangaza wengi katika ulingo wa siasa kwa kuweka bayana kwamba anamuunga mkono rais Uhuru Kenyatta kuwania kiti cha urais mwakani.

Viongozi wa dini ya kislamu kaunti ya Kwale  wameandaa maombi maalumu ya  kuomba mvua  baada ya hali ya kiangazi  kushuhudiwa katika kaunti hiyo kilichosababisha uhaba mkubwa wa chakula katika maeneo ya Kinango na Lungalunga.

Donald Trump amemshinda Hillary Clinton katika matokeo ya uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali.

Wavuvi na wanaharakati wa kulinda mazingira  mjini Amu katika kaunti ya Lamu  wameandamana hii leo kupinga zoezi la uchimbaji wa visima linaloendelezwa na mradi wa Lapset lililoanza wiki tatu zilizopita katika eneo la Shakalapae wakidai uchimbaji huo unaathiri kazi yao ya uvuvi.

Waziri wa elimu Dkt Fred Matiangi amekamilisha ziara yake kaunti ya Kwale kwa kutembelea shule kadhaa za msingi za eneo hilo mapema leo kutathmini hali na jinsi mtihani wa kitaifa wa darasa la nane unavyosimamiwa.

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir amepongeza hatua ya viongozi wa kidini kuandaa maombi ya kuomba mvua kutokana na hali ya ukame inayoshuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini na kusema kwamba tayari dalili ya kukubaliwa kwa dua hiyo imeanza kuonekana.

Hali  ya utulivu imeshuhudiwa katika shule mbalimbali za msingi hapa jijini Mombasa wakati wanafunzi wa darasa la nane wamefanya maaandalizi ya mtihani  wa kitaifa K.C.P.E.

Shirika la mawasiliano nchini limeanzisha shughuli ya usambazaji wa huduma za mitandao kwa shule nne za upili kaunti ya Kwale ikiwa ni kati ya njia moja wapo ya kuthibiti watoto kutumiwa vibaya kingono kupitia mitandao.

Kiongozi wa chama cha Labour  LPK Ababu Namwamba amejipata mashakani baada ya vijana waliojawa na ghadhabu wanaoaminika kuwa wafuasi wa chama cha ODM kumvamia nje ya kanisa la  Glory Worship center Ministry katika eneo bunge la Jomvu kwa kile walichodai kuwa ni msaliti.

Huku uhaba wa chakula ukiendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali Ganze,maafisa wanaohusika na maswala ya lishe bora katika kaunti ya Kilifi wamesema hali hiyo huenda ikasababisha utapia mlo na kudumaa kwa watoto.

Viongozi mbali mbali wa bara la Afrika wamelipokea vyema ombi la Kenya la kuwataka wamuunge mkono waziri wa mambo ya nje Amina Mohammed kuwa mwenyekiti wa tume ya muungano wa nchi za Afrika.

Tume ya kuajiri walimu nchini TSC itawachukulia hatua  za kinidhamu walimu watakaokaidi agizo la kusalia shuleni wakati mtihani wa kitaifa wa darasa la nane na kidato cha nne utakapokuwa ukiendelea.

Idara ya polisi mjini Kilifi imeanzisha uchunguzi kuhusu kisa ambapo babake mwanahabari joseph Masha aliyefariki katika hali ya kutatanisha amejiua kwa kujitia kitanzi nyumbani mwake katika eneo la Kolongoni kaunti ndogo ya Kilifi Kusini.

Rais Uhuru Kenyatta ameagiza idara ya usajili wa watu kuwasijili na kuwapa vitambulisho jamii ya Wamakonde na jamii nyengine za kaunti ya Kwale zisizo na uraia.

Utafiti mpya wa afya unaonyesha kwamba asilimia 92 ya wakenya hawaridhishwi na huduma za afya nchini wakieleza kwamba sekta hiyo iko katika hali mbaya.

Kamati ya bunge juu ya bajeti na makisio imependekeza kupunguzwa kwa idadi ya wabunge katika bunge la kitaifa pamoja na mabunge ya kaunti.

Kamati mbili za bunge zinalitaka taifa la Kenya pamoja na nchi za Afirika mashariki kuiwekea vikwazo nchi ya Sudan Kusini iwapo viongozi wao watashindwa kuelewana kumaliza vita nchini humo.

Hatimaye msafara wa Wamakonde na jamii nyengine zisizokuwa na uraia kutoka kaunti ya Kwale umewasili jijini Nairobi Jumatano jioni baada ya matembezi ya siku tatu.

Wakazi katika eneo la Mariango kaunti ndogo ya Ganze wameanzisha mikakati ya kukabiliana na janga la uhaba wa chakula kwa kuanzisha mradi wa kukamua maji ya alovera na kuuza.

Msafara wa Kundi la Wamakonde, Warwanda na Wapemba uliozuiliwa katika eneo la Voi na funguo na stakabadhi za kuendesha magari kuchukuliwa na polisi wameruhusiwa kuondoka katika kituo cha polisi cha Voi walikopiga kambi ila kutakiwa kesho kufika katika ofisi ya Kamanda wa polisi wa Taita Taveta.

Mahakama kuu ya Mombasa imesimamisha dhamana ya mjane wa marehemu sheikh Rogo kwa muda usiojulikana hadi pale rufaa iliyowasilishwa na afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma itakaposikilizwa.

Kaunti ya Mombasa inatarajiwa kuwa na kinyang’anyiro kikali katika uchaguzi mkuu ujao ambapo gavana Hassan Ali Joho anatarajiwa kupokea ushindani mkali kutoka kwa wapinzani wake.

Utafiti uliofanywa na tume ya maridhiano na utangamano nchini inaonyesha kaunti ya Kirinyaga na Nandi zimeajiri kabila zao peke yake katika kazi zote za kaunti kinyume cha sheria ambapo asilimia sabini inafaa kuwa ya wenyeji na asilimia 30 ya makabila yaliyoko katika kaunti husika.

Mratibu wa serikali ya kitaifa kanda ya Pwani Nelson Marwa ameagiza kutiwa mbaroni kwa gavana wa Mombasa Hassan Ali Joho baada ya kuongoza kundi la vijana wiki iliyopita kubomoa ukuta unaozingira ardhi ya shirika la kitaifa la utangazaji nchini KBC eneo la V.O.K.

Muda mchache baada ya mahakama kumpa dhamana ya shilingi milioni moja mjane wa marehemu Sheikh Aboud Rogo, mahakama imebatilisha uamuzi huo kwa kusimamisha dhamana hiyo kwa muda wa siku nane.

Mwanamume mshukiwa wa wizi ameponea kifo mjini Malindi baada ya kuvamiwa na kupigwa na umma kabla ya kuokolewa na polisi katika mtaa wa Sabasaba.

Bei ya mafuta duniani imeanza kupanda baada ya muungano wa mataifa yanayozalisha mafuta kwa wingi, Opec, kukubaliana kupunguza uzalishaji wa mafuta kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka minane.

Mtu mmoja amefariki baada ya basi la abiria walilokuwa wakisafiria kuhusika kwenye ajali katika eneo la Ziro Ziro huko Kinondo kaunti ya Kwale kwenye barabara kuu ya Likoni-Lungalunga usiku wa kuamkia leo.

Wanawake huko Kwale wameandamana hii leo kukashifu matamshi ya wawakilishi wa wanawake wa kaunti ya Mombasa na Kilifi Mishi Mboko na Aisha Jumwa wakati wa ziara ya kinara wa CORD Raila Odinga wakidai walimdhalilisha Gavana wa kwale Salim Mvurya.

Hatimaye mke wa marehemu Sheikh Samir Khan ameachiliwa huru na kutakiwa kuripoti tena katika afisi za idara ya upelelezi katika kituo cha polisi cha Diani baada ya muda wa majuma mawili huku uchunguzi dhidi yake ukiendelea.

Maradhi ya kisukari yametajwa kuongezeka kwa asilimia kubwa katika eneo la Pwani kutokana na jinsi ya hali ya kimaisha wanayoishi wakaazi wa eneo hili pamoja na aina ya vyakula wanavyotumia.

Shirika la Posta nchini limezindua rasmi huduma zake za M-POST ambapo wateja watapokea jumbe kupitia kwa simu zao kuhusu mzigo au barua watakazotumiwa kupitia shirika hilo.

Watu 2 wamefariki papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya baadaa ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani iliohusisha magari matatu katika eneo la Tiwi kwenye barabara kuu ya likoni-Lungalunga mapema leo katika kaunti ya Kwale.

Timu ya Barcelona kutoka Uhispania itakosa huduma ya mshambuliaji wake matata Lionel Messi kwa kipindi cha wiki 3.

Tume ya huduma kwa mahakama imempendekeza jaji David Maraga kuwa jaji mkuu nchini nafasi iliyowachwa wazi baada ya jaji daktari Willy Mutunga kumaliza muhula wake.

Marekani na Urusi zimelaumiana vikali kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya mashambulizi dhidi ya msafara wa misaada nchini Syria, pamoja na hatua ya kuvunja mkataba wa kusitisha mapigano.

Jarida la soka la Ufaransa limefanya mabadiliko ya kanuni za uteuzi wa mchezaji bora duniani baada ya kushirikiana na FIFA kwenye tuzo za Ballon d’Or kwa miaka 6.

Umoja wamataifa umesitisha misafara yote ya misaada nchini Syria baada ya malori ya Umoja huo kushambuliwa na ndege za kivita karibu na Aleppo Jumatatu.

Mahakama ya kimataifa dhidi ya jinai ICC imeipata serikali ya Kenya na hatia ya kutoshirikiana na mahakama hiyo wakati wa kesi ya rais Uhuru Kenyatta. 

Zaidi ya wanaharakati wa mazingira hamsini wamefanya maandamano kwenye barabara ya Lang’ata kupinga ujenzi wa barabara ya kisasasa ya reli yaani SGR utakaopitia katikati mwa mbuga ya wanyama ya Nairobi.

Mabalozi wa nyumba kumi huenda wakapata sababu ya kujitolea zaidi katika kazi yao hiyo inayohatarisha maisha baada ya serikali kusema itaanza kuwapa marupurupu.

Michuano ya UEFA ndogo au EUROPA imeanza katika hatua ya makundi, mechi 24 zimechezwa ambapo Manchester United ikiwa ugenini ilipokea kichapo cha 1-0 dhidi ya Feyenoord ya Uholanzi.

Tume ya kitaifa kuhusu haki za binadamu nchini KNCHR inatarajiwa kuandaa kikao cha wiki nne kwenye ukanda wa pwani mwezi ujao kwa ajili ya kukusanya malalamishi kuhusu ukandamizaji wa haki za binadamu.

Mwenyekiti wa shirikisho la mpira wa migu la nchini Solvenia Aleksander Ceferin ndio mwenyekiti mpya wa UEFA baada ya kuibuka mshindi dhidi ya mpinzani wake mwenyekiti wa shirikisho la mpira wa migu la Uholanzi Michael van Praag.

Ligi ya klabu bingwa barani Ulaya imeanza usiku wa kuamkia leo, ambapo jumla ya michezo saba kwenye makundi matano ilipigwa kwenye viwanja tofauti. Kundi A Basel ya nchini Uswiz ilitoshana nguvu kwa kutoka suluhu ya 1-1 dhidi ya Ludogorets Razgrad ya nchini Bulgaria.

Zoezi la kutafuta  jaji mkuu nchini  limeanza tena hii leo  huku wakili Lucy Wanja Julius akihojiwa na tume ya huduma kwa mahakama.

Rais Uhuru Kenyatta ameongea kwa njia ya simu na mwenzake wa Tanzania John Magufuli kumpa usaidizi kufuatia tetemeko la ardhi lililoikumba wilaya ya Bukoba iliyopo kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Ndege ndogo ya mafunzo imeanguka katika eneo la Kibiko - Ngong hii leo na kuwaacha mwanafunzi na mwalimu wakiwa na majeruhi.

Mgombea Urais kutoka chama cha Democratic Hillary Clinton amekutwa na ugonjwa wa homa ya mapafu baada ya kuugua katika tukio la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la septemba 11.

Gavana wa kaunti ya Mombasa ametoa wito wa utulivu kwa wakaazi wa jiji la Mombasa baada ya kufeli kwa shambulizi la kigaidi leo asubuhi katika kituo cha polisi cha Central ambapo wanawake watatu washukiwa wa ugaidi wameuliwa na maafisa wa polisi. 

Wanawake watatu washukiwa wa ugaidi wameuwawa na maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Central hapa jijini Mombasa baada ya kuvamia kituo hicho mwendo wa saa nne na nusu asubuhi.

Takriban Mahujaji wa kiislamu milioni 1.5 wamekusanyika nchini Saudi Arabia chini ya ulinzi mkali, kabla ya kuanza rasmi ibada ya hija ya kila mwaka.

Huku mchakato wa kuvunjwa kwa vyama ili kujiunga na chama kimoja cha JAP ukikaribia kukamilika, mbunge wa TNA katika eneo la Narok Kazkazini Moitalel Ole Kenta amekataa kujiunga na chama hicho na kusema ataingia katika chama cha ODM.

Idara ya mahakama imefanya mabadiliko katika baadhi ya mahakama za kadhi nchini ambapo jumla ya makadhi 13 katika mahakama hizo wamepata uhamisho. 

Majaji watatu katika mahakama ya rufaa wametoa hukumu ya kuwaruhusu wanafunzi wa kiisilamu nchini Kenya kuvaa hijab na suruali ndefu kulingana na mafunzo ya dini yao.