Polisi watoa majina ya magaidi waliohusika katika shambulizi la Baure, Lamu

Angazo
Typography

Watu hao  miongoni mwao ni raia wa ujerumani Ahmed Muller ambaye ni kuingo muhimu katika kundi la Al-qaeda na  ambaye pia alihusikia pakubwa katika uvamizi wa Mpeketoni mwaka jana. 

Mwengine ni Ramadhani Kioko maarufu kama Abu Nuseiba ambaye alijiunga na kundi la Al-shabab baada ya kujihusisha na wizi katika jiji la Nairobi. 

Mwaka 2012 idara ya polisi ilisema kuwa  Ramadhani Kioko alifanikiwa kumjumuisha mwanawe mdogo wa mika 10 katika kundi la Al- shabab nchini Somalia. 

Msemaji wa wizara ya usalama wa ndani Mwenda Njika amesema kuwa wengi wa magaidi hao walijeruhiwa katika shambulizi hilo la juzi.