Marufuku ya usafiri kwa wafanyikazi wa nyumbani hadi Saudia

Angazo
Typography

Waziri wa mashauri ya kigeni Amina Mohammed akifika mbele ya kamati ya senate ya usalama amesema japo marufuku ya muda iliyowekwa na serikali ingali ipo bado kumekuwa na ripoti za dhulma za wafanyikazi hao na inanuia kuweka marufuku ya milele. 

Waziri Amina aidha amesema jopo kazi liloteuliwa kuchunguza dhulma hizo pamoja na maofisa wake aidha wamezuru Saudia na kupata ripoti isiyoridhisha ya wakenya na sasa haina nia ya kuendeleza usafirishaji huo. 

Aidha Amina ameeleza kuwa baada ya Eid, serikali ya Kenya na Saudia zinatazamiwa kuweka mkataba wa wafanyikazi wenye taaluma tofauti ambapo baadhi ya makataa ni kuwa sharti kandarasi zote zitafsirirwe kwa lugha ya kiingereza na hati zote za usafiri kuwasilishwa kwa ubalozia wa Kenya Saudia.

 

Kwa sasa kuna zaidi ya wakenya 30,000 wanaofanya kazi Saudi huku 17,000 wakiwa wamejisajili na serikali.