Mke wa marehemu Sheikh Aboud Rogo akamatwa na Polisi

Angazo
Typography

Kulingana na mwanae Munira Aboud Rogo aliyekuwa nyumbani wakati wa tukio hilo amemueleza mwanahabari wetu kwamba maafisa wa polisi zaidi ya kumi wameingia nyumbani mwao baada ya kumpiga askari mlangoni na kisha kumtaka awaitie mama yao ambapo walimkamata na kwenda naye. 

Munira ameeleza kwamba aliwaambia maafisa hao kuwa yeye ndiye mama mwenye nyumba ila wakamwambia awache mzaa na awaitie mke wa Rogo. 

Baada ya mjane huyo Haniya Said Sagar kutoka maafisa hao walimwambia atoke ili wamuoneshe lakiini aliposema hawezi kuondoka wakamwambia kwamba asiwafanyie mambo kuwa magumu bali kuandamana nao. 

Munira ameeleza kwamba maafisa hao walikuwa watano lakini walianza kuongeza mmoja mmoja hadi kufika zaidi ya kumi wakiwa na bunduki wawili wakiwa wanawake. 

Licha ya mtoto huyo kumwambia mamake kwa lugha ya kiarabu kuwa asiwafuate watu hao maana hawaamini mamake hakuweza kufanya hivho kwa sababu maafisa hao walimuamuru kuwafuata. 

Maafisa hao pia walikataa kumpa ruhusa Haniya kumpigia simu wakili wake. 

Watoto wa mjane huyo wamesema hadi sasa hawajui mama yao alipo wala sababu iliyofanywa ashikwe maana kwa muda mrefu maafisa wa polisi hawajawai kufika katika eneo hilo.

Mkuu wa polisi kaunti ya Kilifi Alexendra Makau amethibitisha kuwa wamemkamata na wanamzuilia, ila amedinda kusema sababu ya kumkamata.

LIVE RadioRahma via the App