Hatima ya washukiwa wa ugaidi kujulikana wiki ijayo.

Angazo
Typography

 Pia mahakama itaamua iwapo itawaachilia kwa dhamana wasichana hao, baada ya dhamana yao ya awali kufutiliwa mbali.

Wanne hao ni Ummulkheir Abdullah, Mariam Said Aboud , Khadija Abubakar waliokamatwa eneo la Elwak huku Halima Aden akikamatwa katika Kaunti ya Machakos kwa tuhuma za ugaidi tangu mwaka 2015.

[PICTURE - DAILY NATION]

Hii ni baada ya afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma kutaka hakimu anayesikiliza kesi hiyo kujiondoa na kufutiliwa mbali dhamana yao.

Wiki mbili zilizopita hakimu Henry Nyakweba aliwaachilia wasichana hao kwa dhamana ya shilingi laki tano.

Mmoja wa washukiwa hao, Mariam Said Aboud anakumbwa na ugonjwa hatari wa kumea uvimbe tumboni.

Ikumbukwe kuwa si mara ya kwanza kwa upande wa mashtaka kutaka mahakimu wanaosikiliza kesi hiyo kujiondoa pindi wanapo waachilia kwa dhamana washukiwa hao.

Mwaka jana hakimu Simon Rotich alijiondoa kwenye kesi hiyo baada ya afisi ya mwendesha mashtaka kutokuwa na imani nae katika kesi hiyo.