Mahakama yaongeza tena siku tatu za kujisajili kwa wapiga kura

Angazo
Typography

 Jaji Chacha Mwita ameeleza kuwa usajili huo uliotarajiwa kukamilika leo uendelee hadi baada ya siku tatu.

Uamuzi huo umetolewa baada ya kesi kuwasilishwa mahakamani na mwanaharakati Okiya Omtatah ambaye alitaka zoezi hilo kuendeleya hadi mwezi juni ambapo nimiezi miwili kabla ya uchaguzi mkuu nchini.

Omtatah amewasilisha maswala mengine ambayo yanatarajiwa kusikizwa machi pili ambapo ametaka tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kukubali wakenya kujiandikisha kutumia cheti cha kuzaliwa kwa kuwa wakenya wengi wanachelewa kupewa vitambulisho.

Itakumbukwa kuwa zoezi hilo liliweza kutengewa mwezi mmoja ambao ulitarajiwa kukamilika Februari 14 kabla ya mahakama kuongeza siku mbili ili kuamuwa kesi hiyo.

Aidha jaji huyo amesema kuwa baada ya siku tatu hizo zoezi hilo litafungwa rasmi.