Mahakama ya rufaa yadinda kuwaachilia waliomuuwa Kwekwe.

Angazo
Typography

 Issa Mzee na Veronica Gitahi walipatikana na kosa la mauwaji ya mwendazake Kwekwe Mwandaza mnamo mwaka 2014 huko Kinango.

Jaji wa mahakama ya rufaa Asike Makhandia amesema kifungo walichohukumiwa kinawatosha kuambatana na mashtaka yanayowakabili.

Mwendazake Kwekwe Mwandaza.Awali.

Mahakama pia imetupilia mbali ombi la afisi ya mkuu wa mashtaka ya umma la kutaka wawili hao kufungwa maisha.

Hii ni baada ya pande zote mbili kukata rufaa katika mahakama ya rufaa mwaka jana.

Ikumbukwe mwaka 2015 jaji Martin Muya aliwahukumu kifungo cha miaka saba kila mmoja baada ya kuwapata na hatia ya mauwaji bila kukusudia.