Mahakama yatilia shaka kusimamishwa kazi polisi waliozuia msafara wa raisi.

Angazo
Typography

 Maafisa Barnaba Kimeli na Joel Atuti wanadaiwa kuhusika katika kuziba msafara wa raisi akiwa jijini Mombasa Januri mwaka jana.

Jaji James Rika ametilia uamuzi wa kamati ya nidhamu ambayo iliwasimamisha kazi maafisa hao kwa kuutaja kuwa ulikiuka katiba.

Jaji Rika ameongeza kuwa dereva wa matatu aliandikisha taarifa katika kituo cha polisi cha Makupa na kukanusha kutoa hongo kwa polisi hao.

Amesema kuwa uamuzi uliotolewa na kamati ya nidhamu ya polisi haaukuzingatia ushahidi uliotolewa na dereva wa matatu ambaye alikanusha  kutoa hongo.