Raila arushiwa mawe Turkana Mashariki.

Angazo
Typography

 Vijana hao walikuwa wamejihami kwa sila butu ikiwemo  marungu wakati wa kutatiza ziara hiyo ya Odinga.

Hatua iliyopelekea waandalizi wa mkutano huo kukatiza mara moja.

Odinga ambaye alikuwa ameandamana na gavana wa Turkana Josephat Nanok walikimbia na kueleka eneo la Lokichar ambako walihutubia umma mwengine pasi kutatizwa.

Akizungumza huko Lokichar amesema si vizuri kwa viongozi kuchochea vijana kuzua vurugu,huku akisema kuna viongozi wamehusika katika kuwachochea vijana kubebea mawe ili ktatiza mkutano huo.

Imewalazimu polisi kufyetua risasi hewani ili kuzuia rabsha hizo.

Odinga yuko eneo hilo la Turkana kwa ziara ya siku tatu ambapo anahamasisha jamii kuhusu kujiandikisha kama wapigakura pamoja na kupigia debe muungano wa NASA.