Wahadhiri kuandamana siku ya Jumatatu.

Angazo
Typography

Muungano wa vyuo vikuu UASU,umetangaza kuanza maandamano nchi nzima siku ya Jumatatu baada ya  mazungumzo kushindikana juu ya mkataba wa mwaka 2013-2017.

Muungano wa vyuo vikuu UASU,umetangaza kuanza maandamano nchi nzima siku ya Jumatatu baada ya  mazungumzo kushindikana juu ya mkataba wa mwaka 2013-2017.

Katibu Mkuu wa muungano huo  Constantine Wasonga amesema kwamba  mazungumzo  ya kamati ya Pamoja (JNC),ikiongozwa na waziri wa  elimu Fred Matiangi imeshindwa kutatua matakwa yao. 

Wasonga amesema kwamba jumatatu, jumanne na ijumaa kutashuhudiwa maandamano nchi nzima ambayo hayajashuhudiwa hadi pale matakwa yao yatatuliwa.

Wiki iliyopita muungano huo ulikataa shilingi bilioni 10 zilizotolewa na serikali wakisema ni kidogo mno.

Mgomo huo ulianza Januari 16.