Vijana wawili wauguza majeraha kwa kupigwa risasi na polisi mjini Lamu.

Angazo
Typography

Abdulatif Abdalla  mwenye umri ya miaka 16 na Mohamed Yusuf  mwenye miaka 40 wamepigwa risasi katika maeneo ya Mahakama ya Amu baada  ya vijana kukabiliana na polisi wakati mmoja wao alipohukumiwa kifungu cha miaka 20 gerezani na hakimu mkuu Njeri Thuku kwa makosa ya kupatikana na dawa za kulevya.

Abdulatif amepigwa risasi ya kichwa huku Yusuf akipata jeraha  tumboni.

Kamanda wa polisi kaunti ya Lamu Perminus Kioi amesema wawili hao walijeruhiwa baada ya kundi la vijana kujaribu kuvamia mahakama ili kumuokoa mfungwa aliyehukumiwa kifungo cha miaka 20 kwa kujihusisha na ulanguzi wa dawa za kulevya.

Aidha Kioi amesema polisi watafanya uchunguzi zaidi ili kuwakamata waliohusika na kuwachochea vijana kufanya kitendo hicho.

Vile vile Kioi amesema mafisa wawili wa polisi walijeruhiwa kwa kupigwa na mawe.

Waliofungwa ni Zamzam Mohamed Salim, aliyepigwa kifungo cha miaka 20 Ali Mzee Ali, aliyefungwa miaka 10 naye Wyatham Yusuf almarufu Tima amefungwa miaka 10 pia kwa kosa la kusafirisha na kuuza dawa za kulevya.