Kambi na Maitha wapeleka kampeni zao Ganze

Angazo
Typography

Kulingana na mwaniaji wa kiti cha useneta kaunti ya Kilifi kwa tiketi ya chama cha Kadu Asili Lucas Maitha viongozi wa kaunti hiyo wanajinufaisha binafsi huku wakaazi wakiendeleya kuzama kwenye lindi la umaskini na njaa pamoja na ukosefu wa maji.

Kwa upande wake mwaniaji wa ugavana wa kaunti ya Kilifi kwa tiketi ya chama cha Kadu Asili Kazungu Kambi amesema kuwa atalipa kipau mbele swala la elimu punde tu atakapoingiya mamlakani.

Aidha amesema kuwa haungi mkono mwaniaji yoyote wa kiti cha urais bali amewataka wananchi wa Kilifi kuchagua rais atakayewafanyia maendeleyo.

Wameyasema hayo kwenye mkutano wa kisiasa katika eneo la Matanomane eneo bunge la Ganze.