Shakila akashifu kupigwa risasi watu wawili Lamu

Angazo
Typography

Kwenye mahojiano ya kipekee na mwanahabari wetu Shakila ameitaka mamlaka ya kutathmini utendakazi wa polisi IPOA kuanzisha uchunguzi mara moja akisema maafisa wa polisi wamekuwa wakipiga watu risasi kwa kisingizio cha bahati mbaya.

Wakati huo huo amemtaka rais Uhuru na waziri wa usalama wa ndani kuchukuwa hatua za haraka kukomesha matukio kama hayo huku taifa likielekeya kwenye uchaguzi mkuu ujao mwezi Agosti.

Hata hivyo Shakila ameitaka idara ya mahakama kukabiliana na walanguzi wakuu wa dawa za kulevya na sio watumizi wadogo.

Abdulatif Abdalla  mwenye umri wa miaka 16 na Mohamed Yusuf  wa miaka 40 wanauguza majeraha katika hospitali ya King Fahad baada ya kupigwa risasi katika maeneo ya Mahakama ya Amu ambapo vijana walikabiliana na polisi, baada ya mmoja wao kuhukumiwa kifungocha miaka 20 gerezani na hakimu mkuu Njeri Thuku kwa makosa ya kupatikana na dawa za kulevya.