Mgomo wa wauguzi wagonga siku ya nne leo.

Angazo
Typography

Wakati huo huo mazungumzo kati ya wauguzi na waziri wa leba Philiys Kandie yamefeli tena leo.

Hiyo ni baada ya Kandie kukosa kuhudhuria mkutano wa leo na badala yake leo kushiriki mkutano mwingine na tume ya kutathimni mishahara ya umma SRC. Jana mazungumzo yalifeli baada ya pande husika kukosa kuskizana.

Kandie alikuwa ameahidi huenda muafaka ukapatikana leo.

Wakati huo huo wauguzi wameendelea kususia kazi na kusimama kidete na agizo la wakuu wao la kuendlea na mgomo.

Wagonjwa nao wamezidi kutaabika, hospitali za umma zikisalia bila ya wahudumu wa afya.

 Wauguzi kaunti ya Lamu wameapa kuendelea na mgomo huo hadi pale serikali itakapotekeleza matakwa yao ya nyongeza ya mshahara na marupuru.

Akizungumza na angazo la Rahma kwa njia ya simu katibu mtendaji wa muungano wa wauguzi kaunti ya Lamu Liz Nangu,amesisitiza kuwa watafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa wanachama wao ambao hawashiriki mgomo huo wanaungana na wenzao kuwa na sauti moja kutetea haki yao.

Huko Nairobi Gavana wa Dkt Evans Kidero ametishia kuwachukulia hatua wauguzi wote wanaogoma jijini humo.

Kidero ameshikilia kuwa mgomo huo si halali na kuwataka wauguzi wanaogoma kurejea kazini mara moja.