Kazungu Kambi ashutumu uongozi wa gavana Amason Kingi

Angazo
Typography

Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara huko Mkapuni eneo bunge la Rabai,Kambi amedai kuwa Kingi amekosa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wakaazi wa kaunti hiyo licha ya kupokea fedha kutoka kwa serikali kuu.

Kambi amekosoa matamshi ya gavana huyo ya kumlaumu rais Uhuru Kenyatta katika mikutano ya hadhara huku akimtaka kueleza jinsi alivyotumia fedha zinazoelekezwa kwa kaunti hiyo kutoka serikali ya kitaifa.

Amepuuzilia mbali wito wa viongozi wa ODM waliotoa katika mkutano wao siku ya Alkhamisi katika eneo hilo wa kuwataka wananchi kukipigia kura chama cha ODM katika nafasi zote za uongozi.

Wakati huo huo amekipigia debe chama chake cha Kadu Asili kushinda viti vingi katika uchaguzi mkuu Agosti nane huku akiwarai wananchi kumuunga mkono  rais Uhuru Kenyatta kuchaguliwa tena kutokana na rekodi yake bora ya maendeleo.