Sonko afungwa miezi sita kwa kushindwa kumtafuta mwenyekiti wa MRC.

Angazo
Typography

Hakimu Francis Kyiambia  katika mahakama ya Mombasa ,amemuagiza Sonko kulipa faini ya shilingi  laki moja ama kutumikia kifungo hicho, iwapo atashindwa kulipa faini hiyo kwa muda wa siku 14.

Uamuzi huu unajiri baada ya Mwamnwadzi kukwepa vikao vya mahakama kwa zaidi ya miezi sita kufikia sasa.

Maafisa wa polisi wameshindwa kumkamata Mwamnwadzi licha kutolewa kwa agizo la mahakama kutaka akamatwe.

Sonko amekuwa mdhamini wa Mwamnwadzi pamoja na wenzake tangu kutiwa mbaroni kwao.

Kesi hiyo itatajwa tena Julai 28 mwaka huu.