Washukiwa wanne wa ugaidi wafungiwa korokoroni kwa siku saba zaidi.

Angazo
Typography

Wanne hao wanadaiwa kupanga kutekeleza uvamizi msimu huu wa Ramadhani.

Yayha Salim Bakar anadaiwa kuwa mwalimu wa masjidi Majilis iliyoko eneo la Kikambala.

Wengine wanaokabiliwa na madai hayo ya ugaidi ni Mohammed Masumbuko,Abdalla Ramadhan na Julius Mwandenzi maarufu kama Zinde.

Wote wanashukiwa kuwasajili vijana kujiunga na kundi la kigaidi eneo la Kilifi na Voi.

Watatu kati yao walitiwa mbaroni huko Voi wakiwa na njama ya kusafiri hadi Nairobi.

Hakimu Diana Mochache wa mahakama ya Shanzu ameagiza washukiwa hao kusalia korokoroni kwa muda wa juma moja huku wakifanyiwa uchunguzi.