Visa vya dhuluma za watoto vyaongezeka Ganze.

Angazo
Typography

Idara ya watoto kaunti ndogo ya Ganze imesema kuwa visa vingi vya dhuluma dhidi ya wasichana wadogo vinaendelea kushuhudiwa kila mara eneo hilo.

Idara ya watoto kaunti ndogo ya Ganze imesema kuwa visa vingi vya dhuluma dhidi ya wasichana wadogo vinaendelea kushuhudiwa kila mara eneo hilo.

Afisa mkuu wa idara hiyo Daniel Mbogo amesema kuwa visa tarbani kumi vina ripotiwa kila mwezi.

Kulingana na Mbogo miongoni mwa visa hivyo ni ubakaji sawia na wasichana wadogo kupachikwa mimba.

Mbogo amewataka wazazi kushirikiana na idara hiyo ili kuhakikisha kuwa visa hivyo vimekabiliwa vyema.

Amewalaumu wazazi kwa kuchelewa kuripoti visa hivyo katika afisi husika.