Muuza dawa bila kibali afungwa jela Mombasa

Angazo
Typography

Mwamamke mmoja amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani kwa kosa la kuuza dawa za matibabu bila kibali.

Mwamamke mmoja amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani kwa kosa la kuuza dawa za matibabu bila kibali.

Mary Wafula anadaiwa kuuza dawa hizo mnamo Julai sita mwaka huu katika duka lake alilolipa jina kama county 001 huko Likoni.

Mary amekubali mashtaka hayo mbele ya hakimu mkuu Evance Makori.

Mahakama imemuagiza kutoa faini ya shilingi elfu 50 ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja.