Zabuni ya karatasi za kura yasimamishwa

Angazo
Typography

Uamuzi huu unamaanisha kuwa kandarasi ya uchapishaji karatasi za kura za uraisi iliyokuwa imepewa kampuni  ya Al-Ghurair ilioko nchini Dubai imefutiliwa mbali.

Uamuzi wa jopo la majaji watatu, unailamu IEBC kwa kukosa kuhusisha wananchi katika utoaji wa kandarasi hiyo wakisema ilikuka kanuni za uchaguzi.

Jopo hilo likiongozwa na jaji  Joseph Mativo na George Odunga limeagiza IEBC kuhusisha wananchi kwenye utoaji wa zabuni hiyo upya.

Wameongeza kuwa hawana uwezo wa kubadilisha tarehe ya uchaguzi, hii ikimanisha kuwa tarehe ya uchaguzi itasalia kuwa Agost nane.

Aidha, wamesema IEBC ilikosa kushauriana na wagombea wote wa uchaguzi huo kabla ya kukabidhi zabuni hiyo kwa Al Ghurair ya Dubai.

Mahakama imeamua kwamba kampuni hiyo inaweza kuchapisha karatasi za uchaguzi wa wabunge na maseneta, madiwani na magavana.

Tayari kampuni ya Al-Ghurair ilikuwa imeanza kuchapicha karatasi hizo, ambapo kundi la kwanza la karatasi za kura zinatarajiwa kuwasili humu nchini tarehe 25 mwezi huu.

Majaji hao wamedinda kusimamisha kwa muda uamuzi wao, ili kuipa IEBC na Jubilee kukata rufaa kuhusiana na uamuzi huo.

Hii ni baada ya IEBC na Jubilee kusema kuwa wataka rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama kuu.

Wameongeza kuwa hawaoni sababu kuu ya rufaa hiyo kushinda.

Mahakama imeamua kuwa zabuni hiyo itangazwe upya.