Shakila apinga kuwekwa kwa curfew Lamu.

Angazo
Typography

Kulingana na Shakila njia kuu ya kurudisha hali ya usalama ni kutoa jeshi la Kenya nchini Somalia pamoja na kulinda mipaka yake na sio kuwaekeya wananchi vizuizi vya kutotoka nje kwenye nchi yao.

Ameongeza kuwa serikali imezembeya na kushindwa kwenye vita dhidi ya wanamgambo wa Al shabaab na kuwa inatumia raslimali chungu nzima za nchi huku wakijuwa kwamba wanamgambo hao wako kwenye msitu wa Boni na sio kwenye miji na barabara za kaunti ya Lamu.

Itakumbukwa kuwa hapo jana kaimu waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi aliamuru kuwekwa sheria ya kutotoka nje kwa muda wa miezi matatu katika kaunti za Lamu, Garissa na Tanariver kuanzia leo hii hadi Oktoba 9.

Agizo hilo limeathiri vijiji 15 ambavyo vimeshuhudia hali ya uvamizi mara kwa mara.

Vijiji hivyo ni Holugho , Galmagala, Sangailu, Masalani, Bodhei, Milimani, Baurre, Basuba, Mangai, Mararani, Ijara, Hola, Garsen, Kipini, Kiunga na Ishakani.

Ikumbukwe si mara ya kwanza kwa agizo hilo kuwekwa kaunti ya Lamu, ambapo raisi Kenyatta aliliondoa mnamo mwezi Mei.