Uhuru aionya idara ya mahakama dhidi ya kushirikiana na upinzani

Angazo
Typography

Akizungumza huko Kabartonjo kaunti ya Baringo ameilamu Nasa kwa kujaribu kushinikiza mahakama na tume ya uchaguzi kulemaza shughuli hiyo ya uchaguzi mkuu.

Kauli yake inajiri baada ya mahakama kuu kufutilia mbali zabuni ya uchapishaji karatasi za kura za uraisi iliyokuwa imepewa kampuni ya Al Ghurair.

Wakati huo huo Uhuru na Ruto  wameionya idara ya mahakama dhidi ya kutumiwa vibaya na mrengo wa Nasa ili kulemaza uchaguzi mkuu.

Wawili hao wemesema kuwa mahakama zinatumiwa na NASA, kujaribu kubadilisha tarehe ya uchaguzi na kuchelewesha uchaguzi  ujao.

Kenyatta ametilia shaka kauli ya jaji mkuu aliyeitaka tume ya Ibec kisitisha uchapishaji wa karatasi za uchaguzi wakati ambapo kesi ilikuwa mahakamani.

Raisi ameitaka tume ya uchaguzi kutoshirikiana na upinzani na kuitaka kuwajibika kwa mujibu wa katiba.

Ruto anae ameitaka Iebc kuhakikisha tarehe ya uchaguzi haibadilishwi.

Huku hayo yakijiri tume ya uchaguzi na mipaka IEBC itafanya kikao na wawaniaji wote wa uraisi hapo kesho ilikujadili kuhusu utoaji wa zabani mpya kwa kampuni ya uchapishaji baada ya ile ya kwanza kufutiliwa mbali.

Pia siku ya Jumatano Iebc itafanya mkutano na wananchi ili kutafuta maoni ya mbinu za utoaji zabuni mpya, hii ikiwa ni baada ya mahakama kuu kusema kuwa tume hiyo ilikosa kuhusisha umma katika utoaji wa zabuni iliyokuwa imepewa kampuni ya Al Ghurair.

Uamuzi  wa jopo la majaji watatu ulisema kuwa Iebc ilikiuka kanuni za uchaguzi kwa kutohusisha umma katika utoaji zabuni hiyo.