Raila awarai watu wa Kilifi wampigie kura Agosti nane

Angazo
Typography

Wakiwahutubia wananchi katika eneo la Ganze na uwanja wa water mjini Kilifi viongozi wa muungano huo wamesema kuwa serikali ya jubilee imeshindwa kutimiza ahadi zake kwa wakenya.

Mgombea urais wa Muungano huo Raila Odinga amesema  wakenya wanapitia masaibu mengi kama vile ukosefu wa miundo misingi bora,chakula,matibabu duni miongoni mwa masaibu mengine.

Raila amewarai wananchi wa Kilifi kumpigia kura kwenye uchaguzi mkuu ujao ili aweze kuliongoza taifa hili.

Naye Kalonzo musyoka  amasema kuwa Jubilee imeshindwa kutatua swala la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana wengi eneo la Pwani.

Nao viongozi wa pwani kwenye muungano huo akiwemo gavana wa Mombasa Hassan Joho na mwenzake wa Kilifi Amason Kingi wameilaumu serikali kwa kupanga njama ya kuhamisha bandari hadi Naivasha.