KMYD yazindua mpango wa afya ya uzazi Kilifi

Angazo
Typography

Shirika moja lisilo la kiserikali kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Kilifi limezindua mpango wa miaka mitano ambao unanuia kuimarisha afya ya uzazi katika kaunti hiyo.

Shirika moja lisilo la kiserikali kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Kilifi limezindua mpango wa miaka mitano ambao unanuia kuimarisha afya ya uzazi katika kaunti hiyo.

Shirika la Kenya Muslim Youth Development limezindua mradi huo ambao umebainisha changamoto mbalimbali ambazo zinawakumba wanawake hasa katika afya yao.

Mpango huo umetathmini ukosefu wa zahanati za kutosha katika kaunti hiyo jambo ambalo limewapa wakati mgumu wanawake wajawazito katika kufikia matibabu na hata wakati wa kujifungua.

Afisa mkuu wa shirika hilo Fadhili Msuri amesema kuwa kuboreshwa kwa matibabu kutawapa afya nzuri wanawake na watoto huku akisema kuwa shirika hilo litashirikiana na serikali ya kaunti ya Kilifi katika kuafikia mpango huo.

Naye afisa anayehusika na afya ya uzazi katika kaunti ya Kilifi Esther Mwema amesema kuwa hali ya umaskini imesababisha wanawake na watoto kutokuwa na afya nzuri.