Mahakama kuu yasitisha ununuzi wa ferry mbili mpya .

Angazo
Typography

Jaji Eric Ogola amelitaka shirika la Ferry na kampuni ya utengenezaji ferry ya Ozata Ternasecilik San Ve Tik Limited kusitisha kutengeneza ferry hizo ambazo zinagharimu shilingi bilioni mbili.

Jaji Ogola ameagiza kusitishwa majaribio yoyote ya ferry hizo baharini hadi pale kesi hiyo itakapotatuliwa.

Aidha, shirika la ferry limeagizwa kusitisha kutangaza upya ama kutua zabuni mpya ya ferry hizo hadi kesi iliyowasiliswa kusikilizwa.

Agizo hili limejiri baada ya kampuni ya Bornriz Insurance Marine Surveyors Ltd kuwasilisha kesi hiyo mahakamani baada ya kandarasi yao kufutiliwa mbali na kupewa kampuni ya  ya utengenezaji ferry ya Ozata Ternasecilik San Ve Tik Limited.

Kampuni ya Bornriz Insurance Marine Surveyors Ltd inalilaumu shirika la ferry kwa kukubali ferry hizo kutengenezwa kutumia vifaa duni na vya hali ya chini, kinyume na vile kampuni hiyo ilikuwa imepanga kutumia vifaa vya hali ya juu.

Bornriz Insurance Marine Surveyors Ltd inaishtumu usimamizi wa shirika la Ferry kwa kulipa shilingi milioni 322, ikizingatiwa ferry hizo zinatengenezwa kutumia vifaa duni.

Wakili wa Bornriz Insurance Marine Surveyors Ltd, Gikandi Ngibuini amesema kuwa iwapo ferry  hizo zitatengenezwa kutumia vifaa hivyo basi watumizi wa ferry hizo watahathika pakubwa.