Abdulswamad awataka watu wa Mvita kuepuka siasa za chuki

Angazo
Typography

Akiwahutubia wakaazi wa eneo la Sargoi Timboni mapema leo wakati wa ufunguzi wa barabara ya Cabro Abdulswamad amesistiza umuhimu wa watu wa kuwa na umoja na amani wakati huu wa uchaguzi bila kukubali kugawanywa na wanasiasa kwa misingi ya kikabila au dini.

Aidha amewataka wapinzani wake wa kisiasa kuuuza sera zao kwa wananchi na sio kumtaja yeye kila wanapokwenda huku akiwaomba wakaazi wa eneo hilo kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi mkuu wa Agosti 8 ili waweze kumrudisha mamlakani kwa awamu ya pili.