Gavana Kingi akashifu Kenyatta kwa kuwapotosha watu wa Kilifi.

Angazo
Typography

Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi amekuwa katika maeneo ya Kikambala ambapo amewataka wananchi kupigia kura muungano wa NASA ili kuleta mabadiliko ya hapa nchini.

Kingi amemkashifu vikali rais Uhuru Kenyatta kwa kuwapotosha wakazi wa Kilifi kwa kudai kuwa serikali kuu imeendeleza miradi ya kimaendeleo katika kaunti hiyo.

Amemtaka rais kutotoa vitisho vya kutaka kumfunga kwa madai ya ufisadi kwani hana uwezo kisheria.

Naye mgombea kiti cha ugavana kwa chama cha KADU ASILI Kazungu Kambi ameendeleza kampeni zake katika eneo la Ganze ambapo amewarai wananchi kumpigia kura katika uchaguzi mkuu ujao.