Kingi ataka Kilifi isitajwe kwenye orodha ya kaunti zitakazokuwa na machafuko ya uchaguzi.

Angazo
Typography

Kingi ameeleza kuwa kaunti hii ni eneo lililo na jamii tofauti zinazoishi kwa amani,umoja na ushirikiano thabiti.

Kwenye kikao na wanahabari mapema leo ameeleza kuwa hali hiyo ni ya kuwaogopesha wananchi wa Kilifi kutojikeza ili kupigia kura viongozi wao.

Kingi ameitaka idara ya ujasusi kufanya uchunguzi wake kuhusu madai ya kuweko kwa machafuko badala ya kutangaza kuwa kaunti ya Kilifi haina usalama.

Kwa upande wake  seneta wa kaunti hiyo Stewart Madzayo amewataka maafisa wa polisi kuwapa usalama wananchi badala ya kuwatatiza wananchi kupiga kura.