Abiria wataka mahakama iagize kutumika kwa ferry ya Mv Jambo

Angazo
Typography

Hii ni baada ya mahakama kuu wiki iliyopita kusitisha kutumika na kufanyiwa majarabio feri hiyo hadi pale kesi inayopinga kutumika kwa feri hiyo iliyowasilishwa mbele yake kuamuliwa.

Abiria hao wakiongozwa na Evance Momanyi wameiambia mahakama kuwa wanataka feri hiyo kutumika ili kupunguza msongamano wa abiria na magari katika kivuko hicho.

Wiki mbili ziliyopita kampuni ya Borniz Insurance marine surveyers,iliwasilisha kesi mahakamani kupinga kutumika kwa feri hiyo kwa kusema ilitengenezwa kwa vifaa duni na kuwekwa mitambo  hafifu.

Wakili wa kampuni hiyo Gikandi Ngubuini ameiambia mahakama kuwa feri  hiyo iliwekwa mtambo wa Volvo badala ya Scania kama ilivyotarajiwa.

Gikandi ameitaja hatua ya kutumiwa kwa vifaa na mitambo duni kunaweza kuhatarisha maisha ya wasafiri.

Naye wakili wa shirika la huduma za feri  Nani Mungai amekanusha madai hayo na kusema ferry hiyo ilitengenezwa kwa vifaa na mashihe imara na iko madhubuti kwa kusafirisha abiria.