Mwalimu mkuu wa St.Augustine na wengine wadinda kufunguliwa mashtaka ya mauwaji.

Angazo
Typography

Mwalimu mkuu wa shule ya St. Augustine pamoja na wafanyikazi wengine wanne wamedinda kufunguliwa mashtaka ya mauaji ya mwanafunzi aliyekanyagwa na basi la shule hiyo.

Mwalimu mkuu wa shule ya St. Augustine pamoja na wafanyikazi wengine wanne wamedinda kufunguliwa mashtaka ya mauaji ya mwanafunzi aliyekanyagwa na basi la shule hiyo.

Kupitia wakili wao wakiongozwa na Gikandi Ngubuini, wameiambia Mahakama Kuu ya Mombasa kuwa hiyo ilikuwa ni ajali kama nyengine na hawastahili kufunguliwa mashtaka ya mauaji.

Gikandi ameeleza kuwa itakuwa kinyume cha katiba na ukiukaji wa haki za wateja wake.

Ameitaka afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma kufungua kesi ya kubaini chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo badala ya kuwafungulia washukiwa kesi ya mauaji.

Naye Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya umma tawi la Mombasa, Alexander Muteti amesema sababu ya kifo hicho iko wazi na sharti washukiwa hao kufunguliwa mashtaka ya mauaji.

Mahakama Kuu itatoa uamuzi wake iwapo washukiwa watafunguliwa mashtaka ya mauaji mwendo wa saa nane sawia na jaji Dora Chepkonyi kutoa uamuzi  iwapo atawaachilia washtakiwa hao kwa dhamana.

Siku ya Ijummaa wiki iliyopita mwanafunzi Jeremy Masila, mwenye umri wa miaka sita alifariki baada ya kutumbukia kwenye mwanya wa basi la shule na kukanyagwa na magurudumu ya basi katika eneo la Sega huko Majengo.