Mwalimu mkuu wa St.Augustine na wengine waachiliwa kwa dhamana ya sh.milioni moja.

Angazo
Typography

Watano hao ni mwalimu mkuu wa shule hiyo Kesi Sarah,mhasibu Venant Mwaliko Mwasaru,dereva Valid Mbadi,Fundi Abednego Fundi na manamba Charo Kazungu Charo.

Mnamo Julai 21 asubuhi mwanafunzi huyo kwa jina Jeremy Masila alifariki papo hapo baada ya kutumbukia kwenye mwanya wa basi la shule hiyo eneo la Sega huko Majengo.

Jaji Dora Chepkwonyi ameagiza washukiwa hao kupelekwa katika hospitali kuu ya ukanda wa Pwani ili kuchunguzwa akili kabla ya kufunguliwa mashtaka hayo.

Pia amewaagiza kuripoti katika makao makuu ya afisi za upelelezi iwapo watalipa dhamana hiyo.

Kesi itatajwa Agosti 21 mwaka huu,ili ripoti ya daktari iwasilishwe Mahakamani kabla ya kusomewa  mashtaka.