Kesi ya Seneta Sarai kusikilizwa baada ya uchaguzi mkuu.

Angazo
Typography

Sasa ni wazi kuwa Sarai atagombania kiti hicho pasi kizuizi chochote.

Jaji Erick Ogola amesema hawezi kuhitalifiana na shughuli za uchaguzi kwa sasa.

Hii ni baada ya Hamilton Mwakitale kuwakilisha ombi la kumzuia Sarai dhidi ya kuwania ugavana.

Hamilton anadai kuwa Sarai hawezi kugombea kiti hicho ikizingatiwa bado hajajiuzulu wadhfa wa useneta kufikia sasa.

Kwa upande wake Sarai ameiambia Mahakama kuwa hiyo ni njama ya kisiasa ya kutaka kumzuia kuwania kiti hicho sawia na njama ya kutaka kutatiza shughuli za kampeni yake.

Aidha ameiomba Mahakama kumpa muda wa wiki moja ili kujitayarisha na kesi hiyo.

Kesi hiyo itatajwa Agosti  15 mwezi ujao ,baada ya uchaguzi mkuu.