Mahakama yaagiza kutumika kwa feri mpya ya Mv.Jambo

Angazo
Typography

 Jaji Erick Ogola ameagiza kuletwa kwa feri hiyo ambayo imetengenezwa  nchini Uturuki.

 Wakati huo huo Mahakama imesitisha kutengenezwa kwa nyingine ya pili hadi kesi itakapokamilika.

 Jaji Ogola amelitaka shirika la feri kutotoa zabuni nyengine mpya ya ununuzi wa feri hadi uamuzi wa kesi hiyo utakapotolewa.

 Kampuni ya Bornriz Insurance Marine Surveyors Ltd ilishtaki shirika la feri nchini kwa ununuzi wa feri ambayo inadaiwa kutengenezwa kwa vifaa duni.

 Wakili Gikandi Ngubuini wa kampuni ya Bornriz Insurance Marine Surveyors Ltd amesema atakata rufaa kupinga kutumika kwa feri hiyo.

 Ikumbukwe kuwa shirika la feri nchini liliagiza ununuzi wa feri mbili mpya kutoka nchini Uturuki ili kupunguza msongamano katika kivuko hicho.