Wavuvi wanaoshirikiana na magaidi waonywa Lamu.

Angazo
Typography

Katika kikao na wanahabari mkuu wa oparesheni ya Linda Bondi, Joseph Kanyiri, amesema baadhi ya wavuvi hutumia boti zao kuvukisha magaidi, kuwapelekea vyakula,maji na fedha nyakati za usiku.

Baadhi ya wavuvi wa maeneo ya Ndununi,Rubus,Mabore na Mkokoni ndio wanaodaiwa kuhusika katika kusafirisha magaidi nyakati za usiku.

Ameongeza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaopatikana wakifadhili magaidi hao.

Aidha,amesema kuwa wamefaulu kumtia mbaroni mmoja wa gaidi aliyehusika katika shambulizi la Pandanguo na Jima aliyehukumiwa kulingana na sheria.

Amewasihi wakazi kushirikiana na polisi katika kuwafichua magaidi ili waweze kuishi kwa amani.

Wakati huo huo amewasisitiza wananchi na madereva kutosafiri bila kusindizikwa na maafisa wa usalama ili kuepuka mashambulizi zaidi.

Huku akiongeza kuwa usalama wa wapiga kura umeimarishwa wakiwemo wale waliokatika kambi za wakimbizi wanaotarajiwa kurudi katika vituo walivyoandikisha kupiga kura.