Boti iliyopotea yapatikana, abiria wanne salama.

Angazo
Typography

Maafisa wa ubaharia eneo hilo wamefanikiwa kuliokoa boti hilo likiwa umbali wa maili tatu katike eneo la Kiangwe.

Kulingana na afisa wa shirika la Msalaba mwekundu, Jawthar Alwy, boti hilo lilikuwa linaelekea Faza kutoka Lamu kabla ya kukumbwa na hitilafu ya kimitambo.

Jawthar amesema boti hilo limekarabatiwa katika jeti ya mtangawanda na kuendelea na safari yake.