Viongozi wa kidini Kilifi waunga mkono msimamo wa Nasa

Angazo
Typography

Baadhi ya viongozi wa kidini katika kaunti ya Kilifi wameungana na muungano wa NASA katika msukumo wake wa kumtaka mkurugenzi mkuu wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC Ezra Chiloba kuondoka afisini.
 Viongozi hao wakiongozwa na Rev.Lawrence Nyabiage wa kanisa la Joy Fellowship mjini Mtwapa ,wamesema kuwa Chiloba hawezi kusimamia uchaguzi wa urais kutokana na hitilafu zilizoshuhudiwa.
 Akiwahutubia wananchi wakati wa hafla ya kuwapa shukrani wakazi wa Mtwapa kwa niaba ya mwakilishi wa wadi ya Shimo La Tewa Sammy Ndago,Nyabiage amesema matakwa ya muungano wa NASA ni ya wakenya wote.
 Naye mwakilishi huyo wa wadi amesema kuwa muungano wa NASA unaendeleza kampeni kabambe katika sehemu za mashinani.
 Kulingana na Ndago Raila Odinga atapata kura nyingi zaidi kwani wananchi wa Kilifi wamekubali sera zake za kuwaokoa wakenya kutoka kwa lindi la umaskini.