Ugonjwa wa mapumbu wapungua Pwani.

Angazo
Typography

Utafiti uliofanywa na mashirika matatu ya afya unaonyesha kuwa ugonjwa wa mapumbu umepungua kwa kiasi kikubwa eneo la Pwani.

Utafiti uliofanywa na mashirika matatu ya afya unaonyesha kuwa ugonjwa wa mapumbu umepungua kwa kiasi kikubwa eneo la Pwani.

Utafiti huo umejumuisha shirika la afya ulimwenguni W.H.O,shirika linashughulikia magonjwa yalisioangaziwa zaidi la NTD na taasisi ya utafiti ya KEMRI.

 Akizungumza na wanahabari  katika hoteli moja hapa Mombasa DR Sultan Matendechero amesema kuwa serikali imetoa ufadhili mkubwa kugharamia dawa za ugonjwa huo. 

Vilevile ametoa wito wao kwa wakenya kuzuru vituo vya afya wakati wanaona dalili za maradhi yoyote.

Aidha  Mkurugezi mkuu wa taasisi ya KEMRI kanda ya Pwani  prof  Sammy Njenga  amesema wanashirikiana na mashirika ya afya kote ulimwenguni kuhakikisha kuwa  ugonjwa huo  na magonjwa mengine yaliyosahaulika yakiwemo kichocho yanapungua kufikia mwaka 2020.