Sarai asutwa kwa kujiunga na Jubilee.

Angazo
Typography

Siku ya Jumapili,  Sarai aljiunga rasmi na chama cha Jubilee na kuahidi kuwa atamfanyia kampeni rais Uhuru Kenyatta kwenye marudio ya uchaguzi wa urais Oktoba 26.

Akiwahutubia wafuasi wa NASA kwenye maandamano yao ya kila wiki mbunge wa Likoni Mishi Mboko amemtaja Sarai kama mtu aliyekataliwa kisiasa na kusema kuwa kuhama kwake hakuna athari yoyote.

Adiha Mboko amesisitiza kuwa NASA itasalia kuwa imara katika kaunti ya Mombasa chini ya uongozi wa gavana Hassan Joho.

Naye,aliyekuwa mwakilishi wa wanawake kaunti ya Lamu Shakila Abdalla ameshtumu kuhama kwa Sarai kujiunga na chama cha  Jubilee.

Shakila amesema kwamba kuhama kwa sarai hakutaathiri lolote  chama cha Wiper na muungano wa NASA kwa jumla.

Ameongeza kuwa Sarai hajali maslahi ya wananchi bali kujali maslahi yake binafsi.

Vile vile amesema Sarai amejihadaa kwa kuwa hana kura za kumpa Uhuru Kenyatta baada ya kushindwa katika kinyang’anyiro cha ugavana kwenye uchaguzi wa Agosti nane.