Wafanyikazi 2 wa chuo cha TUM wauwawa kwa kupigwa risasi-Kwale.

Angazo
Typography

Huku watu wengine watatu wakipata majeraha mabaya ya risasi baada ya kushambuliwa na  majambazi katika eneo la Shamu huko Ukunda kaunti ya Kwale.

Wawili hao wameuwawa baada ya kumiminiwa risasi wakiwa ndani ya gari wakiwa pamoja na maafisa wa usalama wanaotoa ulinzi chuoni humo.

Maafisa 2 wa polisi na dereva wa gari hilo wamejeruhiwa na kwa sasa wanapokea matibabu katika hospitali moja eneo hilo.

Akithibitisha tukio hilo ,mkuu wa polisi eneo la Msambweni Joseph Chebusit amesema shambulizi hilo   limetokea sehemu ya msitu wa Mabokoni  ambao wahalifu hujificha na kutekeleza uhalifu.

Haya yanajiri huku wanafunzi wa chuo hicho wakishikilia kwamba hawarudi chuoni humo wakitaka waregeshwe katika chuo kikuu cha Mombasa kwasababu wanahofia usalama wao kwani wako Kichakani.

Ishala Francis ni gavana wa wanafunzi hao.

Mkuu wa Chuo kikuu Cha Mombasa TUM tawi la Kwale Leila Abubakar ameelani tukio la uvamizi huo.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari Leila ameitaka idara ya usalama kufanya uchunguzi mara moja kwani gari hilo limekuwa likisafirisha maafisa hao kila siku kushika doria  shuleni humo.

Wakati huo huo amewahakikishia wazazi kwamba wana wao wako katika mikono ya usalama japokuwa chuo hicho Kiko sehemu ya msitu Mabokoni

Haya yanajiri huku wanafunzi  wa Chuo hicho wakidinda kurudi chuoni humo kwa kile wanachodai kwamba haki zao za kiusalama zimetelekezwa licha ya wao kupaza sauti zao kulilia usalama kwa muda mrefu.