Bunduki iliyoibiwa yapatikana Kwale

Angazo
Typography

Idara ya usalama eneo bunge la kinango kaunti ya kwale  imepata bunduki aina ya AK47 mlangoni kwa chifu wa eneo inayodaiwa kupokonywa maafisa wa usalama eneo la Ukunda.

Idara ya usalama eneo bunge la kinango kaunti ya kwale  imepata bunduki aina ya AK47 mlangoni kwa chifu wa eneo inayodaiwa kupokonywa maafisa wa usalama eneo la Ukunda.

Naibu kamishna wa kaunti ya kwale Mwangi Kahiro amesema kuwa Bunduki hiyo imepatikana eneo la Mnyenzeni huko Kinango.

Amesema  bundiki hiyo ni kati ya bunduki zilipokonywa maafisa wa polisi waliouwawa wakati wa uvamizi katika kanisa la ACK huko ukunda mwezi uliopita.

Kulingana na chifu wa kata ya Kasemeni Benson Kokoi walifanya uchunguzi wa kina baada ya kupata fununu kutoka kwa wakaazi kwamba kulikuwa na kijana aliyekuwa anamiliki bunduki kutoka mtaa wa mnyenzeni.