Walipatikana na mifuko ya plastiki kizimbani Mombasa

Angazo
Typography

Kumi na moja hao walitiwa mbaroni katika maeneo tofauti jijini Mombasa hapo jana.

Peter Chacha, Micheal Nyawa na John Mwita walitiwa mbaroni wakiwa na mifuko hiyo katika soko kuu la Kongowea wakifungia miwa.

Mumo Ngangi, Timothy Mwiti, Katoi Mangi na Martin Musila walishikwa eneo la Buxton wakiwa wamefunga matunda ya Apple wakitumia mifuko hiyo.

Naye Adan Mohamed, Mwepa Jawa, Benson Munyoki na Amos Mumo wakitiwa mbaroni eneo la Mwembe Tayari wakiwa na mifuko hiyo.

Kumi na moja hao wamekubali mashtaka hayo mbele ya hakimu Martin Rabera.

 Mwendesha mashtaka kutoka shirika la kudhibiti mazingira la NEMA,Janet Alango ameitaka mahakama kuwahukumu kwa kifungo washukiwa hao kwa kukiuka agizo lla kupinga marufuku utumizi wa mifuko ya plastiki.

Lakini Hakimu Rabera amewaachilia huru washukiwa hao,huku akiwapa onyo kali la kutopatikana na mifuko hiyo iliyopigwa marufuku.