Mtoto wa miaka minne atumbukia kwenye shimo na kufariki Jomvu

Angazo
Typography

Kulingana na aliyeshuhudia mkasa huo ambaye hakutaka kutajwa jina,  mtoto huyo alikuwa akicheza na wenzake juu ya shimo hilo ambalo lilikuwa limefunikwa na mabati kabla ya kutumbukia ndani yashimo hilo.

Juhudi za wanajamii kumuokoa mtoto huyo hazikufua dafu kwani baada ya kumtoa kutoka kwa shimo hilo mtoto huyo alikuwa ameshaaga dunia.

Chifu wa eneo hilo chifu Matano amethibitisha tukio hilo na kulitaja kama la bahati mbaya.