Idadi ya watoto wa kuranda randa yaongezeka Mombasa

Angazo
Typography

Katika mahojiano ya kipekee na mwanahabari wetu Nzenge ameihusisha hali hiyo na joto la kisiasa linaloshuhudiwa nchini pamoja na wazazi kukosa kuwajibikia  majukumu yao na badala yake kujihusisha na masuala ya siasa na maandamano na hivyo kupelekea watoto wengi kutaka  kujitegemea maishani.

Nzenge amesema idara yake inapania kuanzisha zoezi la kuwatambua watoto wote wa kurandaranda na kuwarudisha shuleni ili kuona kwamba watoto hao wanafaidika na haki ya kupata elimu kama watoto wengine nchini.

Aidha ametoa wito kwa viongozi wa dini mbalimbali kuwajibika na kuanzisha mikakati ya kuwatoa watoto hao mtaani na barabarani.