Serikali yaapa kuunga mkono mabadiliko ya sheria ya Wakf

Angazo
Typography

Muigai ameeleza kwamba sheria ya wakfu ya mwaka 1951 imepitwa na wakati na imekuwa haisaidii kivyovyote jamii ya waisilamu kama ilivyotarajiwa na waisilamu waliotoa mali yao kwa ajili ya umma.

Maneno yake yameungwa mkono na kiongozi wa wengi bungeni Adan Duale ambaye amesema anasubiri ripoti hiyo iundwe mswada ndio aweze kuhimiza wabunge wenzake kuupitisha.

Baadhi ya Marekebisho hayo ni kumuondoa mratibu mkuu wa pwani kuwa kamishna, makamishna wote kuwa wasomi wa fani mbali mbali kulingana na nafasi zilizopo, kumuondoa Kadhi kuwa kamishna, kuwepo kwa kitengo cha sheria na kitengo cha ardhi kitakachofanya kazi na tume ya ardhi, wizara ya ardhi na serikali za kaunti.

Kikao cha kupitia ripoti ya marekebisho ya ripoti ya jopo hilo inaendelea jijini Nairobi.

Wengi wa wajane na mayatima walengwa wa mali ya wakf wanaendelea kukosa usaidizi huku mali chungu nzima za wakf zinazofaa kuwasaidia zikiendeleya kufaidiwa na wachache.