Jumanne yatangazwa kuwa siku ya mapumziko nchini

Angazo
Typography

Hii ni kwa ajili ya kutoa nafasi kuapishwa kwa rais mteule Uhuru Kenyatta kwa awamu ya pili.

Kuapishwa kwa Uhuru ni kufuatia kutupiliwa mbali kwa kesi zilizowasilishwa mahakamani kupinga ushindi wake siku ya Jumatatu.

Mkuu wa watumishi wa umma Joseph Kinyua ameeleza kuwa Uhuru anatarajiwa kuapisha Jumanne kuanzia saa nne asubuhi katika uwanja wa kimataifa wa Moi Kasarani jijini Nairobi.

Uwanja huo ambao rais anatarajiwa kuapishwa juma lijalo sasa umo mikononi mwa jeshi. 

Hapo jana wanajeshi walifanya mazoezi ya hafla hiyo wakiwa na sare kamili. 

Maandalizi ya kuapishwa kwa rais ambaye atakuwa akihudumu muhula wake wa mwisho yamefikia kilele huku kamati ya maandalizi ikiwatarajia zaidi ya wageni elfu mia moja kuhudhuria hafla hiyo.