Mahakama kuu yadinda kumuachilia huru mshukiwa wa ubakaji.

Angazo
Typography

Mahakama kuu ya Mombasa imetupilia mbali rufaa ya mwanamume aliyefungwa kifungo cha maisha, anayedaiwa kumbaka na kumpachika ujauzito mtoto mwenye umri wa miaka 15.

Alargic Jembe anadaiwa kumbaka na kumpachika mimba mtoto huyo kati ya Januri na Septemba mwaka 2014 katika eneo la Kisauni.

Akitupilia mbali rufaa hiyo jaji Njoki Mwangi amesema kuwa ushahidi unaonyesha kuwa mshtakiwa alimbaka mtoto huyo.

Jaji huyo ameagiza mshtakiwa kuendelea na kifungo chake cha maisha kwa mujibu wa katiba.