Ustadh adaiwa kuwanajisi wanafunzi katika madrasa moja Bakarani

Angazo
Typography

Ustadh Idi Ali anadaiwa kuwanajisi na kuwalawiti zaidi ya wanafunzi kumi wa madrasa hiyo katika tarehe mbali mbali kisa cha hivi karibuni kikiwa cha msichana wa miaka 7 ambaye anaendelea kuuguza majeraha baada ya kunajisiwa.

Kulingana na Mohammed Salim ambaye mtoto wake ni miongoni mwa watoto walionajisiwa, ustadh huyo amekuwa akikifanya kitendo hicho kwa muda mrefu licha ya wazazi kutojua kwani ustadh huyo amekuwa akiwatishia wanafunzi hao kuwa atawachinja iwapo watafichua siri hiyo.

Ustadha Khadija Mbarak ambaye ni ustadh mwenza katika madrasa hiyo amesema baada ya kuwachunguza baadhi ya wanafunzi alibaini kuwa ustadh huyo alikuwa na tabia ya kuwanajisi wanafunzi hao.

Mbarak amesema yeye binafsi aliweza kupokea malalamishi kutoka kwa wanafunzi 8 mbali na wengine ambao wanaogopa kujitokeza.

Aidha amedai kuwa sio mwanzo kwa mwalimu huyo kutekeleza kitendo hicho kwani amewai kufukuzwa kutoka madrasa kadhaa hapo awali kwa sababu iyo hiyo.

Aidha Mbarak ametoa wito kwa idara ya polisi kumsaka haraka iwezekanavyo ustadh huyo ambaye ameingia mafichoni tangu kuibuka kwa siri hiyo siku ya Jumamosi ili kumkamata kabla hajakimbilia sehemu nyingine na kufungua madarasa mpya.

Wengi wa wazazi waliofuatwa na mwanahabri wetu walihofia kunakiliwa sauti zao kwasababu sizizoeleweka na mwanahabari kunyimwa fursa ya kukutana na watoto wanaodaiwa kunajisiwa na kulawitiwa.

Kisa hicho kilibainika siku ya Jumamosi baada ya msichana wa miaka 7 kupatikana kuvuja damau katika sehemu zake sa siri kabla ya kudai kunajisiwa na Ustadh huyo ambapo baadaye wanafunzi zaidi walijitokeza kufichua visa vyao.