Utafiti:Wanafunzi wa darasa la 5 na 6 washindwa kufanya masomo ya darasa la nne.

Angazo
Typography

Utafiti mpya wa elimu unaonyesha kuwa wanafunzi wa darasa la tano na sita katika kaunti 10 hawawezi kufanya masomo ya darasa la nne.

Utafiti huo ulifanywa na shirika la Twaweza East Afrika wakishirikiana na shirika la Uwezo Kenya kati ya Julai mwaka jana na Julai mwaka huu.

Kaunti ambazo wanafunzi hawawezi kufanya masomo ya darasa la nne ni kaunti ya  Laikipia, Garissa, Mandera, Kirinyaga, Kiambu, Embu, Nakuru, Nairobi, Kisii na Baringo.

Kulinagana na afisa wa shirika la Twaweza, Francis Njuguna wanafunzi wa darasa la tano na sita walianguka masomo ya darasa la nne hasa somo la  Kiengereza na Hesabati .

Aidhda,amesema kuwa wanafunzi wa shule za umma hawafanyi vyema kwenye masomo ya kiengereza na hesabati ikilinganishwa na shule za kibinafsi.

Ametaja ukosefu wa vifaa bora katika shule za umma kuwa chanzo cha wanafunzi kukosa kufanya vyema,ikilinganishwa na shule za kibinafsi ambazo zinavifaa bora.