Mume amuuwa mkewe kisa ni shilingi 50.

Angazo
Typography

Polisi jijini Nairobi wanachunguza kifo cha mwanamke mwenye umri wa miaka 40 ambaye amefariki kutokana na majeraha yanayodaiwa kutokana na kichapo alichopokea kutoka kwa mumewe wiki mbili zilizopita.

 Kulingana na polisi shida ilitokea pale mume alipomshtumu mkewe huyo kwa kumuaibisha kwa kuomba shilingi hamsini kutoka kwa jirani alizotumia kununua mboga ya omena ambayo waliitumia kwa ajili ya chakula cha chajioni.

Polisi wamesema mwanamke huyo alikuwa ametoka kujifungua wiki mbili zilizopita na alikuwa hana nguvu za kutosha mwilini kustahimili kichapo hicho.

Mbali na mashtaka hayo mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 38 anashatakiwa pia na kumbaka mwanawe wa kike mwenye umri wa miaka 14 mtoto huyo alipojaribu kumsaidia mamake.

Mwanamke huyo alifariki katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta alipokuwa akipokea matibabu na polisi wamepewa wiki mbili kukamilisha uchunguzi wao kabla ya kumwasilisha mshukiwa kortini kwa mashtaka ya mauaji na ubakaji.